BALOZI DKT NCHIMBI : UJUZI WA RASIRIMALI WATU NI NGUZO MUHIMU KATIKA TAASISI ZA AFYA.

  Timothy Marko | DmNewsOnline

         DAR ES SALAAM

TAASISI  za afya nchini zimetakiwa kuendelea kujenga uwezo wa rasilimali watu ili kuimarisha uwezo wa taasisi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya.

Wito huo umetolewa leo, Julai 16, 2026, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt
 Emanuel Nchimbi, wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Nchimbi amesema afya ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa, kwani rasilimali watu yenye afya ndiyo msingi wa ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu.

Amesema Hayati Rais Benjamin Mkapa alitambua umuhimu wa kuimarisha sekta ya afya kama njia ya kujenga rasilimali watu na kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini.

"Taasisi ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kukuza na kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu, jambo lililochangia kuimarisha uwezo wa taasisi mbalimbali za afya," amesema Dkt. Nchimbi.

Amesisitiza kuwa ili sekta ya afya iweze kutoa huduma zenye ufanisi, ni muhimu kuwaandaa viongozi wa kada za afya kitaaluma na kuwajengea uwezo wa kusimamia taasisi kwa ufanisi.

Pia ameeleza kuwa vijana wanapaswa kupewa kipaumbele katika kujengewa uwezo wa kitaaluma ili kuhakikisha kunakuwepo kizazi chenye uwezo wa kuendeleza na kuimarisha taasisi za afya.

Kwa upande wake, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation imefanikiwa kujenga viongozi imara na kuendeleza rasilimali watu katika sekta ya afya.

Amesema kama mrithi wa maono ya Hayati Benjamin Mkapa, ataendelea kuhakikisha malengo na dira ya Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation yanaendelezwa na kufikiwa.

"Tunapotafakari urithi wa Hayati Benjamin Mkapa, tunatafakari pia umuhimu wa kuandaa viongozi wenye uwezo wa kuimarisha taasisi zetu," amesema Dkt. Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, amesema Afrika inaendelea kukabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu, hali inayoongeza mahitaji ya watumishi wa afya wenye ujuzi na weledi.

Amesema uwekezaji katika maendeleo ya rasilimali watu katika sekta ya afya ni muhimu ili kuhakikisha huduma bora zinapatikana na kukidhi mahitaji ya wananchi yanayoendelea kuongezeka. 



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO