Posts

MAPATO MANISPAA TABORA YAPAA

Image
   Na Allan Kitwe,DmNewsonline                     TABORA  HALMASHAURI ya manispaa Tabora imeendelea kupiga hatua kubwa kimaendeleo ikiwemo kufanikisha utekelezaji miradi ya maendeleo kutokana na kasi nzuri ya ukusanyaji mapato kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali. Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Dkt John Pima alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao cha Baraza la madiwani. Amefafanua kuwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027 wanatarajia kukusanya zaidi ya sh bilioni 12 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali ikiwa ni sehemu ya rasimu ya mapendekezo ya bajeti yao kwa mwaka huu wa fedha. Amedokeza kuwa mapendekezo hayo ni ishara ya kazi nzuri ambayo imeendelea kufanywa na timu yake ya mapato kwa mwaka wa fedha uliopita ambapo walipanga kukusanya kiasi cha sh bilioni 8.6 na kupata mafanikio makubwa.  Dkt Pima amefafanua...

TUME YA PDPC KUANZA UKAGUZI WANAOKIUKA SHERIA ULINZI WATAARIFA BINAFSI.

Image
  Timothy Marko DmNews Online          DAR ES SALAAM.   TUME ya Taarifa Binafsi  Nchini (PDPC)imesema kuwa itaanza kufanya Ukaguzi wa Taasisi za umma na Binafsi zinazochakata,kuhifadhi nakusafirisha taarifa binafsi nje ya Nchi pasipo kuzingatia Sheria ya Ulinzi wa taarifa Binafsi Sura ya 44 na kanuni zake. Akizungumza Leo January 22,2026 jijini Dares Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt.Emanuel Mkila amesema kuwa hatua zitachukuliwa kali za kisheria kwa mtu yeyote au Taasisi itakayokiuka sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi sura ya 44 katika Utekelezaji wa Shughuli zake. "Hatua hizo nipamoja na kutozwa faini,kifungo au vyote na kulipa Fidia watakao athirika kutokana na matakwa ya sheria"Amesema Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Dk.Emanuel Mkila. Dkt.Mkila Ameongeza kuwa Taasisi itakayo bainika kuvunja Faragha kutumia taarifa Binafsi bila ridhaa ya Mhusika wa taarifa hizo. Amesisitiza kuwa Taasisi hiyo inatoa wito kwa taasisi Binafsi na Umma kuchukua hatua...

‎BoT YAWAHIMIZA WANANCHI KUTUMIA TAASISI ZA FEDHA ZILIZOSAJILIWA

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsTz Tanga ‎Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewahimiza wananchi kuhakikisha wanachagua na kutumia huduma za taasisi za fedha zilizosajiliwa rasmi na benki hiyo ili kujilinda dhidi ya hatari za kifedha na kuchangia ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. ‎ ‎Wito huo umetolewa na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)  kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Mwile Kauzeni, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho  ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea kitaifa mkoani Tanga. ‎ ‎Kauzeni amesema kuwa wananchi wanaotaka kupata mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi wanapaswa kwanza kuzitambua taasisi za fedha zilizosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kutembelea tovuti rasmi ya BoT ya www.bot.go.tz, ambako kuna orodha ya benki, taasisi nyingine za fedha pamoja na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (bureau de change). ‎ ‎Amesema kuwa mwananchi anatakiwa kuwa makini katika kuchagua...

TARURA YATENGA BIL 7 KUTENGENEZA KM 114 ZA BARABARA TABORA

Image
    Na Allan Kitwe, DmNewsonline                  TABORA  WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoani Tabora wanatarajia kutengeneza barabara zenye urefu wa km 114.05 kwa gharama ya sh bilioni 7.4 katika Wilaya ya Tabora Mjini kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Hayo yamebainishwa  na Meneja wa Wakala huo Wilaya ya Tabora, Mhandisi Subira Manyama alipokuwa akiwasilishwa rasimu ya mapendekezo ya bajeti ya TARURA kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Ametaja vipaumbele vya rasimu hiyo kuwa ni kukarabati barabara zote ambazo zimekuwa hazipitiki kwa kipindi kirefu ili ziweze kupitika wakati wote, kuzifanyia matengenezo barabara zote za mjini na vijijini ili ziwe imara zaidi. Ameongeza kuwa watafanya matengenezo ya kawaida kwa sehemu korofi zote na ya muda maalumu kwa baadhi ya barabara ili kuwezesha wananchi kusafiri na kusafirisha mazao yao kutoka vijijini kwenda kwenye masoko kwa mwaka mzima. Mhandisi Manyama amefafanua kuwa ...

TIRA: BIMA SI HIARI, NI MGUZO YA KULINDA UCHUMI NA MAISHA YA WANANCHI

Image
Na Mwandishi Wetu, DmNewsTz Tanga  Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Kaskazini, Dkt. Emmanuel Lupilya, amesema kuwa suala la bima si la hiari bali ni nguzo muhimu na injini ya kulinda maisha ya wananchi, shughuli za kilimo, uchumi wa mtu mmoja mmoja pamoja na uchumi wa taifa kwa ujumla. Dkt. Lupilya ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea mkoani Tanga kuanzia Januari 19 hadi 26, 2026, alipokuwa akizungumza baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba, kutembelea banda la TIRA. Amesema mamlaka hiyo haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya makampuni ya bima yatakayokiuka miongozo, sheria na taratibu zilizowekwa, kwani kufanya hivyo kunakwamisha maendeleo ya sekta ya bima na uchumi kwa ujumla. “Hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa makampuni yatakayokiuka miongozo, sheria na taratibu tulizoweka kama mamlaka, kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma maendeleo,” amesema. Ameeleza kuwa TIRA, kwa...

WAUMINI KANISA LA SHINCHEONJI WADAI UWEPO WA HUJUMA DHIDI HA UHURU WA DINI KOREA KUSINI

Image
Na Mwandishi wetu, DmNewsTz Korea Kusini Serikali imelenga waziwazi kundi maalum la kidini, ikiliita "madhara ya kijamii" na "hatari" huku ikihamasisha mamlaka ya serikali kwa njia ya kulipiza kisasi.  Vitendo kama hivyo ni ukiukwaji mkubwa wa Kifungu cha 20 cha Katiba ya Jamhuri ya Korea, ambacho kinahakikisha uhuru wa dini na kanuni ya kutenganisha kanisa na serikali. Shincheonji Kanisa La Yesu linaonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu kuingiliwa kwa upande mmoja na mamlaka ya serikali na linahimiza sana utawala kuzingatia kanuni za utawala wa haki, uliozuiliwa, na wa kikatiba. Mnamo Januari 12, Rais Lee Jae-myung alisema wakati wa mkutano na viongozi wa kidini kwamba "madhara ya kijamii [yanayosababishwa na dini fulani] yamepuuzwa kwa muda mrefu sana, na kusababisha uharibifu mkubwa."  Hii ilifuatiwa mnamo Januari 13 na Waziri Mkuu Kim Minseok , ambaye, wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri, alitumia maneno kama vile "uongo" na "uzushi" k...

SELF YATOA ELIMU YA MTUMIZI SAHII YA MIKOPO KWA WANANCHI

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsTz  Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa SELF, Linda Mshana, amesema mfuko huo unaendelea kutoa elimu sahihi,kwa wananchi kuhusu matumizi bora ya mikopo, mambo ya kuzingatia kabla ya kuchukua mkopo pamoja na maswali muhimu ya kuuliza Yanayohusiana na taasisi za kifedha, ili kuepuka changamoto ya mikopo ya riba kubwa inayodaiwa kuwanyonya wananchi. Mshana ameyasema hayo leo Januari 20, 2026, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Usagara, jijini Tanga.  Maadhimisho hayo yalianza Januari 19 na yanatarajiwa kumalizika Januari 26, 2026. Amesema mfuko wa SELF unawakaribisha wananchi wote wa mkoa wa Tanga kufika katika maadhimisho hayo ili kupata elimu sahihi ya fedha pamoja na kufahamu fursa mbalimbali zilizopo zitakazowawezesha kujiendeleza kiuchumi. Ameeleza kuwa SELF ina mikopo ya aina mbalimbali ikiwemo mikopo kwa wafanyabiashara wa sekta ya nafaka, wafugaji, wavuvi na wakulima.  Aidha, kuna mikopo y...