TUME YA PDPC KUANZA UKAGUZI WANAOKIUKA SHERIA ULINZI WATAARIFA BINAFSI.
Timothy Marko DmNews Online
DAR ES SALAAM.
TUME ya Taarifa Binafsi Nchini (PDPC)imesema kuwa itaanza kufanya Ukaguzi wa Taasisi za umma na Binafsi zinazochakata,kuhifadhi nakusafirisha taarifa binafsi nje ya Nchi pasipo kuzingatia Sheria ya Ulinzi wa taarifa Binafsi Sura ya 44 na kanuni zake.
Akizungumza Leo January 22,2026 jijini Dares Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt.Emanuel Mkila amesema kuwa hatua zitachukuliwa kali za kisheria kwa mtu yeyote au Taasisi itakayokiuka sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi sura ya 44 katika Utekelezaji wa Shughuli zake.
"Hatua hizo nipamoja na kutozwa faini,kifungo au vyote na kulipa Fidia watakao athirika kutokana na matakwa ya sheria"Amesema Mkurugenzi Mkuu wa PDPC Dk.Emanuel Mkila.
Dkt.Mkila Ameongeza kuwa Taasisi itakayo bainika kuvunja Faragha kutumia taarifa Binafsi bila ridhaa ya Mhusika wa taarifa hizo.
Amesisitiza kuwa Taasisi hiyo inatoa wito kwa taasisi Binafsi na Umma kuchukua hatua za kujisajili ilikuweza kulinda Faragha ilikuweza kuelekea Uchumi wa kijitali.
"T umesi
nasisitiza kuwa kipindi ni Dirisha la Mwisho la Muda wa hiari kabla ya hatua kali hazijachukuliwa kwa mtu ama Taasisi atakaye vunja sheria"Amebainisha Dkt,Mkila. 


Comments
Post a Comment