Posts

RC TABORA KUPELEKA MASHABIKI WA SOKA UWANJA WA TAIFA

Image
     Na Allan Kitwe, DmNewsonline                        TOBORA MKUU wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameahidi kukodi mabasi ya kutosha ili kupeleka mamia ya mashabiki wa soka wa Mkoa huo uwanja wa Taifa ili kushangilia timu ya taifa (Taifa Stars) kwenye ufunguzi wa michuano ya CHAN. Ametoa ahadi hiyo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alieleza kuwa Mkoa huo ni miongoni mwa Mikoa yenye hamasa kubwa na mashabiki wengi wa soka hapa nchini. ‘Mashindano haya yapo nchini kwetu, ni lazima tupeleke mashabiki wengi zaidi kuliko Mikoa mingine ili kuiongezea hamasa timu yetu ya taifa, nitakodi mabasi ya kutosha ya kupeleka mashabiki bure uwanja wa taifa na kuwarudisha’, amesema. ‘Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa zawadi nono kwa vijana wetu wakitwaa ubingwa, na sisi tutamuunga mkono kwa kuipa hamasa kubwa timu yetu ya taifa ili ifanye vizuri na kutwaa ubingwa ’, amesema...

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA BIL 38 TABORA

Image
         Na Allan Kitwe,DmNewsonline                           TABORA MWENGE wa Uhuru unatarajiwa kuwasili Mkoani Tabora kesho Julai 26 ili kuangazia maendeleo ya wananchi, ukiwa Mkoani hapa utazindua miradi yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 38.8. Akizungumza  na vyombo vya habari, Mkuu wa Mkoa Paul Chacha amesema kuwa ukiwa Mkoani hapa utatembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika Wilaya zote 7. Amebainisha kuwa utapokelewa katika uwanja wa mpira wa shule ya sekondari Tura, iliyopo Wilayani Uyui, Mkoani hapa ukitokea Mkoa wa Singida na kuanza kukimbizwa maeneo mbalimbali katika Wilaya hiyo. Ameongeza kuwa Julai 27 mwenge wa uhuru utakimbizwa katika Wilaya ya Kaliua na kisha Wilaya za Urambo, Sikonge, Tabora manispaa, Igunga, Nzega Mji  na kuhitimisha mbio zake katika Halmashauri ya Nzega DC. Baada ya kuhitimisha m...

ADB YATOA DOLA MILIONI 5.2 KUTOKOMEZA UGAIDI, FEDHA HARAMU.

Image
    NaTimothy Marko DmNewsonline         DAR ES SALAAM. BENKI ya Maendeleo ya Afrika ADB imeingia ya Dola milioni 5.2  makubaliano na Taasisi ya Taasisi ya inayoshughulika na Kudhibiti wa Fedha Haramu ilikuweza kutokomeza Vitendo vya Ugaidi Sambamba na Rushwa. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mara Baada ya Makubaliano hayo Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Sauda Msemo amesema kuwa Fedha hizo linalenga Kudhibiti Vitendo vya Fedha Haramu zinazo tumika katika kufadhili Vitendo vya Ugaidi. "Mpango huu unajumuisha Nchi za Madagascar Rwanda Burundi na Msumbiji "Amesema Naibu Gavana wa Benki kuu Sauda Msemo. Pia  Katika hatua nyingine Muwakilishi Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB Tanzania Patricia Laverly amesema Tanzania imekuwa ikipiga hatua Katika Kudhibiti Vitendo vya Utakatajishaji fedha Sambamba na Ugaidi. Aidha, Mtalamu waUchumi  Sera nautawala Bora katika Ukanda wa kusini Mwa Afrika Kalamu Gebreselas...

CHAUMMA WAPOKEA MAPENDEKEZO KWA KAMATI JINSI YAKUPATA WANAWAKE WAWAKILISHI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline            DAR ES SALAAM  KATIBU Mkuu wa Chama cha Umma(CHAUMA),Salim Mwalimu amepokea maependekezo ya sifa na vigezo vya wanawake wanaotarajiwa kupata nafasi ya uongozi wa Viti Maalum kwa nafasi ya Udiwani,Wawakilishi wa Ubunge. Mapendekezo hayo  yamewasilishwa Leo Julai 24,2025 Katika Ofisi za Chama Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Kamati ,Moza Ally wa kamati aliyoiunda kama mtendaji Mkuu wa Chama. Akizungumza  na waandishi wa habari mara baada yakupokea mapendekezo hayo Katibu Mkuu CHAUMMA Salim Mwalimu amewata wanawake kutojielekeza kwenye Viti Maalum kwani wanawake Wanauwezo wakushinda kwenye majimbo hivyo wajitokeze kushindana kwenye majimbo kwani CHAUMMA wameweka utaratibu kwa wanawake kufikiriwa. "Katika Kamati iliyoundwa kutoa mapendekezo iliangalia utaratibu, sifa  na vigezo vya udiwani wa Viti Maalum anaetoka CHAUMMA,Uwakilishi wa Viti Maalum na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani...

WAZIRI MKUU AMALIZA ZIARA BELARUS, ANADI FURSA ZA UWEKEZAJI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                          BELARUS                     WAZIRI  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa ametumia ziara yake nchini Belarus kunadi fursa za uwekezaji katika maeneo manne ya kipaumbele ya Serikali ya awamu ya sita ambayo ni kilimo, afya, madini na ulinzi & usalama. Mhe. Waziri Mkuu katika siku mbili za ziara yake,  tarehe 22 na 23 Julai 2025 ametembelea kampuni kubwa nane zenye nguvu ya mitaji jijini Minsk na kuzihakikishia utayari wa Serikali ya Tanzania kushirikiana nazo kwa kuzipatia kila aina ya msaada zitakapokuja Tanzania kuwekeza. Kwenye eneo la kilimo, Mhe. Waziri Mkuu alikutana na viongozi wa kampuni ya AFTRADE ambayo tayari ipo nchini na kuwasisitiza kuongeza kasi katika kuendeleza kilimo hususan kuwa na programu za kuwasaidia wakulima wadogo mitaji, utafiti na mafunzo ili kilimo...

INEC YAWATAKA WASIMAMIZI,MAWAKALA KUFANYA KAZI KWA WELEDI.

Image
Na Timothy MarkoDmNewsonline              DAR ES SALAAM  TUME ya Uchaguzi Huru ya Uchaguzi Nchini (INEC) imewataka Mawakala na Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktober Mwakahuu Kuzingatia Maadili ya kusimamia Uchaguzi ikiwemo Kutunza Siri na kusimamia Maadili ya Viapo vyao Katika Uchaguzi. Akizungumza Katika Mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwakahuu Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Balozi Omar Ramadhani Mapuri amesema kuwa Mafunzo hayo yanalenga kuwaelimisha na kutilia Mkazo Juu ya Sheria za Uchaguzi za Madiwani,Wabunge na Rais ya Mwaka 2024. "Sheria hizi zinalenga kukuza uelewa Juu ya Usimamizi wa kura,Nakutoa Majukumu sahihi ya Wasimamizi wa Uchaguzi"Amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Balozi Omar Ramadhani Mapuri. Balozi Omar Ramadhani Mapuri Ameongeza kuwa Wasimamizi hao wa Uchaguzi Mkuu wanatakiwa kuyatafusiri Mafunzo hayo kwa Vitendo. Amesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu unaotara...

NEEMA YAWASHUKIA WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA

Image
  Na Allan Kitwe,DmNewsonline                    TABORA  SERIKALI ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imepongezwa kwa kupanua wigo wa soko la zao la tumbaku hali ambayo imechochea wakulima kuongeza uzalishaji na kuwa na uhakika wa masoko. Pongezi hizo zimetolewa na Meneja Mkuu wa WETCU 2018 Ltd Samwel Jokeya alipokuwa akizungumza  na Mwandishi wa mndao huu wa DmNewsonline  aliyetaka kujua mafanikio ya wakulima wa tumbaku wa Mkoa huo katika miaka 4 ya Rais Samia. Amesema kuwa changamoto za wakulima wa tumbaku katika miaka 4 ya uongozi wake zimepungua sana na masoko ya zao hilo na mazao mengine sasa ni ya uhakika tofauti na miaka mingine, na tumbaku yote inayozalishwa sasa inauzwa.  ‘Hadi sasa tuna jumla ya makampuni 21 nchini yaliyoidhinishwa kununua zao la tumbaku yakiwemo ya wazawa, hali hii imeongeza ushindani wa bei, wengine wanalipa hadi dola 3 kwa kilo, hiki ndicho wanachotaka wakulima...