RC TABORA KUPELEKA MASHABIKI WA SOKA UWANJA WA TAIFA


     Na Allan Kitwe, DmNewsonline

                       TOBORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameahidi kukodi mabasi ya kutosha ili kupeleka mamia ya mashabiki wa soka wa Mkoa huo uwanja wa Taifa ili kushangilia timu ya taifa (Taifa Stars) kwenye ufunguzi wa michuano ya CHAN.

Ametoa ahadi hiyo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alieleza kuwa Mkoa huo ni miongoni mwa Mikoa yenye hamasa kubwa na mashabiki wengi wa soka hapa nchini.

‘Mashindano haya yapo nchini kwetu, ni lazima tupeleke mashabiki wengi zaidi kuliko Mikoa mingine ili kuiongezea hamasa timu yetu ya taifa, nitakodi mabasi ya kutosha ya kupeleka mashabiki bure uwanja wa taifa na kuwarudisha’, amesema.

‘Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa zawadi nono kwa vijana wetu wakitwaa ubingwa, na sisi tutamuunga mkono kwa kuipa hamasa kubwa timu yetu ya taifa ili ifanye vizuri na kutwaa ubingwa ’, amesema 

Chacha ameeleza kuwa Mkoa huo ni wa tatu kwa ukubwa nchini hivyo watatumia wingi wa idadi ya wananchi wake kupeleka hamasa kubwa zaidi kwenye mechi ya ufunguzi itakayopigwa Agosti 2 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ametoa wito kwa mashabiki wa soka kutoka Wilaya zote 7 za Mkoa huo walio tayari kwenda kushuhudia ufunguzi wa michuano hiyo kujitokeza kwa wingi ili kujaza mabasi, usafiri wa kwenda Jijini Dar es salaam na kurudi ni bure.

Akiongea kwa niaba ya mashabiki wenzake, Nico Joseph mkazi wa manispaa Tabora amemshukuru Mkuu wa Mkoa na kuahidi kuwa wako tayari kwenda uwanja wa Taifa kuishangilia timu yao kwenye mtanange wa ufunguzi wa michuano hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO