CHAUMMA WAPOKEA MAPENDEKEZO KWA KAMATI JINSI YAKUPATA WANAWAKE WAWAKILISHI
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu wa Chama cha Umma(CHAUMA),Salim Mwalimu amepokea maependekezo ya sifa na vigezo vya wanawake wanaotarajiwa kupata nafasi ya uongozi wa Viti Maalum kwa nafasi ya Udiwani,Wawakilishi wa Ubunge.
Mapendekezo hayo yamewasilishwa Leo Julai 24,2025 Katika Ofisi za Chama Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Kamati ,Moza Ally wa kamati aliyoiunda kama mtendaji Mkuu wa Chama.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada yakupokea mapendekezo hayo Katibu Mkuu CHAUMMA Salim Mwalimu amewata wanawake kutojielekeza kwenye Viti Maalum kwani wanawake Wanauwezo wakushinda kwenye majimbo hivyo wajitokeze kushindana kwenye majimbo kwani CHAUMMA wameweka utaratibu kwa wanawake kufikiriwa.
"Katika Kamati iliyoundwa kutoa mapendekezo iliangalia utaratibu, sifa na vigezo vya udiwani wa Viti Maalum anaetoka CHAUMMA,Uwakilishi wa Viti Maalum na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Viti Maalum anaetoka CHAUMMA",amesema
Aidha,amesema kwamba kamati ilikuwa na wanawake ambao walishawahi kuwa Wabunge na Madiwani katika nafasi mbalimbali za kisiasa.
Pia amesema kwamba Uteuzi wa Viti Maalum unatakiwa kuwa wa wazi,Shirikishi na jumuishi kama jambo linawahusu wanawake hivyo wapewe nafasi wanawake wenyewe kwa mapendekezo pamoja na kutoa ushauri kwa Chama namna ya kupata wagombea kwa nafasi za wanawake 











Comments
Post a Comment