INEC YAWATAKA WASIMAMIZI,MAWAKALA KUFANYA KAZI KWA WELEDI.


Na Timothy MarkoDmNewsonline

             DAR ES SALAAM 


TUME ya Uchaguzi Huru ya Uchaguzi Nchini (INEC) imewataka Mawakala na Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktober Mwakahuu Kuzingatia Maadili ya kusimamia Uchaguzi ikiwemo Kutunza Siri na kusimamia Maadili ya Viapo vyao Katika Uchaguzi.

Akizungumza Katika Mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwakahuu Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Balozi Omar Ramadhani Mapuri amesema kuwa Mafunzo hayo yanalenga kuwaelimisha na kutilia Mkazo Juu ya Sheria za Uchaguzi za Madiwani,Wabunge na Rais ya Mwaka 2024.

"Sheria hizi zinalenga kukuza uelewa Juu ya Usimamizi wa kura,Nakutoa Majukumu sahihi ya Wasimamizi wa Uchaguzi"Amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Balozi Omar Ramadhani Mapuri.

Balozi Omar Ramadhani Mapuri Ameongeza kuwa Wasimamizi hao wa Uchaguzi Mkuu wanatakiwa kuyatafusiri Mafunzo hayo kwa Vitendo.

Amesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktober Mwakahuu wa Marais, Wabunge, na Madiwani unafanyika kwamujibu wa Sheria.

"Natoa Maelekezo kuwa  Ubandikaji wa Mabango na Orodha ya majina yanabandikwa ipasavyo kwa mujibu wa Sheria"Ameongeza Balozi Omar Ramadhani Mapuri.

Balozi  Mapuri Amesisitiza kuwa Maelekezo yanayohusu Uchaguzi Mkuu Nilazima yakapitia vyombo vya Habari.

"Hakikisheni mnatunza Siri Ukiukwaji wa Kutunza Siri nikinyume cha Sheria"Alibainisha Balozi Omar Ramadhani Mapuri.

Balozi Mapuri Alitia mkazo kuwa Nilazima Watendaji wa Uchaguzi Mkuu kuu kuhakikisha  Asasi za kirahia zinazo shiriki kwenye Mchakato wa Uchaguzi ikiwemo Uangalizi wanafuta Sheria za Uchaguzi.

" Katoeni Mafunzo hayakwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu kwa WELEDI" Amebainisha BaloziOmari Mapuli.

Kwaupande wake Mratibu wa Mafunzo hayo Selemani Katiti amesema kuwa katika Mafunzo hayo Jumla ya Mada (11) ziliweza kutolewa kwa waratibu wa Mikoa ,Pamoja Wasimamizi wa Uchaguzi ikiwemo Maadili ya wagombea , Maadili ya Wasimamizi wa Uchaguzi Sambamba na taratibu za kuhesabu kura kituoni.

Amesema kuwa Mada nyingine ni Pamoja na Gharama za Uchaguzi Ambapo maada hizo ni Dira kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktober Mwakahuu.

"Mambo haya tutazingatia kama Dira tunaahidi kuyatekeleza, Naomba tukatende Haki ndio dhamana tuliyo pewa" Amesema Mratibu wa Mafunzo Selemani Katiti.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO