MABAKI YA MWILI WA MTANZANIA JOSHUA MOLLEL YAWASILI NCHINI TANZANIA

 Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

MABAKI  ya mwili wa Kijana Joshua Mollel aliyeuwawa nchini Israel na wapiganaji wa HAMAS Oktoba 07, 2023 yamewasili leo Novemba 19, 2025 katika kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).

Mabaki ya mwili huo yamepokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania ukiongozwa na  Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa na Balozi Silima Haji Kombo. 

Mabaki ya Kijana Joshua Mollel yanatarajiwa kuzikwa   kesho  Novemba 20,  2025 mtaa wa Njiro, katika kata Orkesumet Wilaya ya Simanjiro,  Mkoani Manyara.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO