MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE AAHIDI UJENZI WA KITUO CHA KISASA STENDI YA DALADALA TEMEKE MWISHO

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM MGOMBEA Ubunge Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Wakulima(AAFP),Yusuph Rai amesema kwamba endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025 atahakikisha Temeke Mwisho kunajengwa kituo kikubwa Cha daladala chenye hadhi na thamani ya Wilaya ya Temeke pamoja na kituo kitakachounganisha magari yanayokwenda Mikoa ya Kusini ili kuongeza thamanj ya mapato ya Jimbo Hilo. Amezungumza hayo leo Septemba 15,2025 katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Temeke zilizofanyika katika Viwanja vya Tandika Sokoni kata ya Tandika Jijini Dar es Salaam. Aidha ,amesema kwamba soko la Tandika ndio kariakoo ya Temeke,hivyo akipata nafasi ya kuwa mbunge atahakikisha soko hilo kuwa kubwa na liwe la kimataifa pamoja na kuishawishi serikali ili Soko hilo liwe kitovu cha biashara. Pia amesema kwamba Tandika imekuwa na changamoto ya maji safi na salama kwa siku nying...