JAMII IMETAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI BORA YA IMANI

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

            DAR ES SALAAM 


JAMII imetakiwa kulea watoto katika misingi ya Imani pamoja kuzingatia haki za binadamu hii inawajenga watu wote  katika misingi bora yenye hofu ya Mungu bila kujali dini.

Masuala ya malezi katika misingi ya kidini ni eneo muhimu  linaloanzia katika familia,tulee watoto wetu katika misingi ya Imani itawajenga watoto kutambua uwepo wa watu wengine lakini pia kuwa na ufahamu wa kutambua mipaka yake namna anavyoabudu lakini pia malezi ni msingi muhimu sana wa kuleta amani katika jamii.

Hayo yamebainishwa   Septemba 27,2025 na Mwenyekiti  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ,Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) wakati wa kutoa mada ya Haki za binadamu katika Mkutano Mkuu wa 54 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania unaoendelea Kitonga Kata ya Msongola Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaaam ,

Amesema kwamba jukumu la msingi la  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni taasisi simamizi ya kitaifa ambayo inasimamia masuala ya haki za binadamu na masuala ya utawala Bora lakini pia ni mchunguzi maalum kwa masuala ya utawala Bora.Tume imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na vilevile imetungiwa Sheria Sura 391 ya Sheria za nchi,kikatiba na kisheria Tume hii imepewa majukumu ya kusimamia na kulinda hifadhi ya haki za binadamu na uzingatiwaji wa misingi ya utawala Bora katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hii ikiwa na maana kwamba jukumu la msingi pamoja na kupokea malalamiko kutoka kwa wanannchi ambao haki zao zimevunjwa au misingi Yao ya utawala Bora imekiukwa

"Tunapozungumzia misingi ya utawala Bora tunazungumzia inavyokiukwa maana yake Kuna viongozi wa serikali ama taasisi nyingine za umma ambao wanatekeleza majukumu Yao kwa kukiuka misingi Ile ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora",amesema Mwenyekiti Mwaimu

Aidha ,amesema  haki ya kuabudu nchini mwetu ni Moja ya haki za kimsingi za binadamu zinazolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mikataba mingine ya kimataifa,haki hii ya kuabudu imetamkwa katika katika Ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatoa uhuru kwa mtu binafsi kuamini,kuabudu na kushiriki katika dini au Imani anayoichagua bila kulazimishwa au kubaguliwa,uhuru wa mtu vilevile kubadilisha Imani,uhuru wa mawazo ,Imani na dhamiri,kufundisha dini au kueneza dini bila kuingiliwa na mtu yoyote  na anaweza kufanya hivyo peke yake,faragha au kuwashirikisha wengine kama ilivyokuwa katika mkutano huu unaoendelea Toka Jana Leo na kesho.

"Nafurahi kwamba shughuli zinazotekelezwa na Jumuiya hii za kuendeleza amani,upendo,ushirikiano pamoja nakuhimiza utu wa Sheria kwa dini zote,kuhimiza adabu,maadili mema kupitia mafundisho ya dini ya Kiislamu kutoa huduma za jamii kama vile maji na elimu zote zinzohusiana na ulinzi na uzingatiaji wa haki za binadamu

Hata hivyo ,amesema kwamba kumekuwepo  na changamoto ya kuwepo uvunjaji wa haki za binadamu,kimsingi inatokana na tabia mbalimbali za watu kutopenda kuheshimiana pamoja ma kuzingatia misingi ya maisha.

"Watu kuwa na mawazo makubwa zaidi kuliko mwingine ni maeneo ambayo yanaweka mazingira ambayo yanasababisha mtu mwingine aguse haki ya mtu mwingine bila sababu za msingi,Kila mmoja ahakikishe anajua mipaka yake ni kwamba ukiona Kuna mwelekeo wa kuleta vurugu basi wewe utakuwa mtu wa kurudi nyuma ,lazima kwanza utamuweka Mungu wako mbele hakuna jambo ambalo wewe uende ukavunje haki ya mwingine",amesema

Kwa upande wake Msemaji  wa Jeshi la Polisi ,DCP David Misime amewataka viongozi wa dini ya kiislamu wote waliokusanyika katika mkutano wa 54 kufundishana umuhimu wakutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa sababu kuna mambo ambayo tunayashuhudia kwenye  mitandao ya kijamii,sasa hivi ambayo hayapaswi kutamkwa,kuandikwa wala kusambazwa na mtu ambaye ana mafundisho ya kweli ya Mwenyezi Mungu iwe upande wa waislamu,iwe upande wa wakristo kama kweli umeisoma Quran na imekuingia huwezi kutamka,huwezi kuandika na huwezi kusambaza maneno ambayo yapo kwenye mitandao ya kijamii,sasa hivi nasisitiza kuangalia watoto wao,vijana wao tufundishane  namna Bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii,tukitumia vizuri inatunufaisha  na  utakuwa na maisha mazuri kwa sababu yatakupa elimu mbalimbali lakini pia yatakuwezeha wewe kujiendeleza kiuchumi kwa sababu utatangaza biashara yako,kilimo chako na kitu chochote kile  kitakupa maarifa ya Dunia hii

Aidha ,amesema kwamba Jumuiya hiyo ya Ahmadiyya wanapoendelea na mkutano wao waendelee kuliombea Taiafa liweze kufanya uchaguzi wake kwa amani,utulivu,upendo na usalama ili baada ya uchaguzi,Taifa liendele kubaki salama,amani,utulivu,upendo,usalama na mshikamano.

Pia kuendelea kukemea na  kufundishana ndani ya familia  juu ya kufuata Sheria zinazohusiana na  uchaguzi ili basi tusije kufikia mahali tukasigana na Sheria,tukisigana na Sheria inakua sio jambo jema,lakini pia nimewaambia umuhimu wa kutunza amani kwa sababu amani usipoitunza hata kile kidogo ulichonacho kidogo ambacho unaona wewe ni kidogo hutaweza kuwa nacho kikikutoka mkononi kwa sababu utakuwa ni mkimbizi wa ndani au mkimbizi wa nje",amesema Misime

Naye mmoja wa wanajumuiya wanaoshiriki  katika mkutano huo kutoka Mtwara ,Asmahani Nassor amesema wamejifunza mambo mengi hasa ya kiroho lakini pia mada zilizofundishwa za kujua umuhimu wa haki za binadamu na mada hizo zimetujenga na kutambua umuhimu wa watu wenye uhitaji maalum,lakini pia kuwatunza wazazi wetu wanapokua katika umri wauzee tuweze kuwajali kama walivyotujali sisi tulivyokuwa wadogo.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.