HUNGARY KUWEKEZA UPATIKANAJI WA MAJI ZIWA VICTORIA .

  Timothy Marko DmNewsonline 

       DAR ES SALAAM.

KATIKA kuhakikisha Sekta ya Maji inaimarika serikali  kwa Kushirikiana na Nchi ya Hungary imeingia makubaliano ya kuboresha Maeneo ya Ukanda wa Ziwa Victoria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mara baada makubaliano hayo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabiti Kombo amesema Makubaliano hayo ya Dola milioni 55 za kimarekani yanalenga kukuza Sekta ya Maji Uwekezaji wafedha hizo kutawezesha Makampuni mbalimbali kutoka Hungary kuwekeza Nchini Tanzania.

"Makubaliano haya ya Leo yatawezesha Makampuni kutoka Hungary kuja kuwekeza Nchini Tanzania"

 AmesemaWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Mahamoud Thabiti Kombo.

 Balozi Thabiti Kombo Ameongeza kuwa Sambamba na Makubaliano ya Uwekezaji wa Makampuni kuwekeza Nchini Tanzania pia Nchini hiyo imeingia makubaliano na Nchi ya Tanzania Kuboresha Sekta ya Elimu kwakukuza ziara za kimasomo ilikuwezesha Wanafunzi wa vyuo kuweza kukuza ujuzi na uzoefu.

"Sambamba na hayo mapema hii Leo tunakwenda kuzindua Ubalozi wa Hungary Masaki Jijini Dar es Salaam Tanzania" Alibainisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabiti Kombo.

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchini HungaryPeter szijjaro amesema kuwa Ushirikiano wa Nchini ya Hungary ni wakipindi cha Takriban miaka 50 .
Amesema Hungary imekuwa mdau Muhimu wa Masuala mbalimbali ya kiusalama Kimataifa, Ambapo Tanzania nimdau Muhimu katika kuboresha Hali ya Usalama katika Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki.

"Changamoto kwa Nchi Africa nyingi ni Upatikanaji wa Majisafi na Salama "Amesema Wa Mambo ya Nje Nchini Hangary Peter szijjaro.

Aidha, kwaupande wake Rais wa Taasisi Chember ya Wafanyabiasha Nchini TCIAA Vincent Minja amesema Ushirikiano wa Hungary na Tanzania kutawezesha kukuza Ujuzi wa Masuala mbalimbali ya Akili mnemba na kuboresha Kilimo.   



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.