ELIMU YAENDELEA KUTOLEWA KWENYE BANDA LA BoT




Na Richard Mrusha,DmNewsOnline
Geita

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Zena Ahmed Said, ametembelea Banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.

Akiwa kwenye Banda la BoT, ameshuhudia wananchi wakipewa elimu kuhusu masuala ya fedha, ikiwemo jinsi ya kuwekeza fedha zao.

Amesema kuwa kuna watu wengi wenye fedha, lakini hawajui jinsi ya kuziwekeza. Hata hivyo, kupitia maonesho haya wanapata fursa ya kufundishwa namna ya kuwekeza kwenye dhamana za Serikali ambazo huwapatia faida kubwa, tofauti na kuwekeza sehemu zisizo rasmi.

Ameongeza kuwa wananchi watembelee banda hilo ili wafundishwe jinsi ya kujiepusha na utakatishaji wa fedha, kwa sababu ni suala linaloweza kuiingiza nchi kwenye matatizo makubwa.

Amesema kuwa elimu inayotolewa hapo inalenga masuala ya kifedha pamoja na mengine mengi ya kifedha, na inatolewa bure. Hivyo, wananchi wanapaswa kufika kwa wingi ili wasikose fursa hiyo muhimu ya kielimu.

Ameongeza kuwa kwa ujumla amefurahishwa na maonesho hayo ambayo, mbali na wachimbaji na wadau wa madini, pia yameshirikisha wajasiriamali kutoka Tanzania Bara na Visiwani, pamoja na wale wanaotoka nje ya mipaka ya Tanzania. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani nchi yetu ina utulivu, amani na upendo.



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.