DC KOMBA AIPONGEZA BoT
Na Richard Mrusha,DmNewsOnline
GEITA
Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba
Ameipogeza BoT kwa namna ambavyo wameendelea kuelimisha Umma kuhusu taasisi yao kwa wananchi wanaotembelea Banda Hilo ndani ya viwanja vya Samia Suluhu Hasan kwenye maonesho ya nane ya Teknolojia ya Madini Mkoani geita.
Komba amepata Fursa ya ya kuzungumza na watumiahi wa Benki na Miongoni mwa akitengo alichotembelea ni kitengo cha usimamizi wa masuala ya fedha ,usimamizi wa masusla ya benki na mikopo
Amesema Kumekuwa na changamoto kubwa sana kwenye maeneo yetu juu ya uwepo wa taasisi ambazo hazijasajiliwa na kutoa mikopo kwa riba kubwa Zaidi ,zinawafilisi wananchi kwa kutofuata taratibu
Amesema BoT wanancho kitengo maalum ambacho kazi yake ni kuhakikisha kwamba kunakuwa na taasisi zinazotoa mikopo kwa wananchi zikiwa zimesajiliwa na zikiwa zinazingatia sera za kifedha za Taifa letu kwa ujumla.
Amesema Moja ya jambo kubwa lililomfurahisha nikuona namna ambavyo BoT inazibiti taasisi zinazotoa mikopo inayoumiza,(kausha damu ) na kutoa mikopo bila kuwa na usajili wa namna yoyote ile.
amesema ni wajibu wao kama Serikali kuwasiliana na BoT kwa kupitia kitengo chao cha uchunguzi waanze kuchukua hatua mbalimbali na ikiwemo kuchukua hatua kali Zaidi kwa hizo kampuni au taasisi zinazotoa huduma za kifedha na hazijasajiliwa na zinawaumiza wananchi.
Ameongeza kuwa kwa pamoja tunaweza kuwalinda wananchi wetu
Kumekuwa na manung’uniko katika maeneo mbalimbali kwa wananchi wetu yanayohusu kukopeshwa fedha na kulipa kwa riba kubwa ndani ya mwezi mmoja,wapo baadhi ya wajane nyumba zao zimeuzwa lakini tukafanya mawasiliano tukakuta taasisi zile hazijasajiliwa Amesema Komba,:
Ametoa Rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kwenda kukopa fedha kwenye taasisi ambazo zimesajiliwa na zinatambuliwa na BoT ili kama kuna changamoto yoyote iwe ni rahisi wa wenzetu wa BoT kuchukua hatua kumlinda mtumiaji wa taasisi hizi za kifedha.




Comments
Post a Comment