KOMBA ATO RAI KWA DIB KUENDELEA KUPANUA WIGO



Na Richard Mrusha,DmNewsOnline
Geita

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, ametoa rai kwa Bodi ya Bima ya Amana kuendelea kupanua wigo wa huduma zake ili kuhakikisha mitaji ya Watanzania, hususan katika vikundi vidogo vya kifedha kama SACCOS na VICOBA, inabaki salama. 

Hayo ameyaema Leo Sep 26,2025 wakati wa Ziara ya kutembelea Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini Mkoani geita   amesaema Watanzania wengi bado wanawekeza fedha katika maeneo ambayo hayajasajiliwa rasmi, hali inayowaletea hasara kubwa pale vikundi hivyo vinapovunjika.

Amesema   kuwa katika ofisi za wakuu wa wilaya, mara kwa mara wananchi wamekuwa wakifika kulalamikia kupoteza akiba kubwa walizowekeza Unampokea mwananchi anakwambia amewekeza milioni 30 kwenye kikundi cha kifedha lakini zote zimepotea. Tunaanza kuhangaika kumtafuta kiongozi wa kikundi bila mafanikio. Ni wakati sasa wa kuongeza kasi ya kuhakikisha mitaji ya Watanzania inalindwa.

Ameongeza kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapaswa kushirikiana kwa karibu na Bodi ya Bima ya Amana kushuka chini kwa kasi kubwa ili kufikia taasisi ndogo ndogo.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa Bodi ya Bima ya Amana, Lwaga Mwambande, amesema Kwa niaba ya DIB amepokea ushauri  wa Mkuu wa Wilaya ya Geita na kusisitiza kuwa ushirikiano na wadau wengine wa sekta ya fedha utaendelea kuimarishwa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanakuwa na imani katika mfumo rasmi wa kifedha nchini.

Mwambande amasema kuwa kwa sasa kinga inayotolewa na bodi hiyo ni Shilingi milioni 7.5 kwa kila mteja endapo benki itafungwa. “Kinga hii inawafikia wananchi wengi kwani asilimia 99 ya wenye amana wanalindwa. Hii inatupa nafasi ya kuendelea kuwahakikishia Watanzania usalama wa fedha zao katika taasisi za kifedha zilizosajiliwa,” amasema

Hata hivyo, Mwambande amekiri kuwa bado ipo haja ya kuangalia namna bora ya kufikia vikundi vya kifedha visivyo rasmi, kama vile VICOBA na SACCOS, ili kuhakikisha Watanzania wanaotumia mifumo hiyo pia wananufaika na ulinzi wa mitaji yao.

Ameongeza kuwa pamoja na jukumu la kuwalipa fidia wananchi endapo benki ikifungwa, lengo kubwa la Bodi ya Bima ya Amana ni kujenga imani ya kudumu kwa wananchi kuhusu mfumo wa kifedha. 

“Tukiendelea kujenga imani, wananchi wataendelea kutumia mfumo wa fedha rasmi, jambo ambalo litachochea ukuaji wa uchumi wa taifa,” amesema Mwambande.



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.