WABUNGE ZAIDI 40 WASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 14 WA AFRIKA WA JUKWAA LA UTAWALA WA MTANDAO


Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

              DAR ES SALAAM 


NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,Eng.Maryprisca Mahundi amefungua kikao Cha awali Jukwaa la Utawala wa Mtandao Barani Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Mei 29,2025 Jijini Dar es Salaam amesema kwamba zaidi ya wabunge 40 toka nchi mbalimbali za Afrika wamehudhuria mkutano .

Naibu Waziri Mahundi amesema kwamba kikao hicho ni maandalizi kuelekea ufunguzi rasmi wa mkutano unaotarajiwa kufunguliwa Mei 30,2025 unaohusu masuala ya Utawala wa Mtandao ambapo mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Aidha ,ameeleza kwamba serikali imejipanga kwa kuthibiti matumizi yasiyosahihi ya mitandao kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

"Wakati wa chaguzi mbalimbali wapo baadhi ya watu wanatumia vibaya mitandao hasa kudhalilisha wanawake kwahiyo wameonya kuwa hawatavumilia kwani sheria itachukua mkondo wake",amesema

Pia ameeleza kwamba kipindi cha chaguzi wanawake wamekuwa wakidhalilishwa hivyo serikali iko imara na imejipanga vizuri ,tutadhibiti wale wote watakaotumia vibaya mitandao na niwatake vijana watumie vizuri mitandao tulinde nchi yetu.

Ameongeza kuwa ndani ya Wizara yetu tunaendeleza vijana kwa kuibua vipaji kwa watoto wa shule za Msingi na Sekondari kwa kuendeleza mashindano mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na TCRA kwa watoto wa kike hivyo tumejenga vituo vya kukuza bunifu vinaendelezwa na Tume ya Tehama nchini na vituo nane vinaendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali.

Hata hivyo ameeleza kwamba katika mkutano huo watajadili kwa upana masuala ya intaneti kwa mustakabali mzima wa Taifa letu kwa kushirikiana na nchi nyinggine A Afrika ili kuhakikisha jamii inaendelea kupata uelewa wa masuala ya intaneti

Kwa upande wake Mkurugenzu wa Miundombinu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhandisi Leo Magomba amesema kuwa kuna fursa mbalimbali zinazopatikana  kupitia mtandao kwa hiyo ni wajibu wetu kuhakikisha kutumia vema mitandao ili tuweze kunufaika

Mkutano huo wa jukwaa utawakutanisha wadau mbalimbali kutoka nchi za Afrika na Tanzania ndio mwenyeji   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO