NLD HAWATASHIRIKIANA NA VYAMA VINGINE VYA SIASA

Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

                 DAR ES SALAAM 

CHAMA Cha National League for Democracracy kimetangaza rasmi kutoshirikiana na chama chochote kile Cha siasa ila kitashiriki uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Maamuzi hayo yametokana na kwamba NLD ni mhanga wa mashirikiano yaliyofanywa mwaka 2015 walipoingia kwenye mashirikiano na vyama vya siasa nchini yaliyopachikwa jina la UKAWA.

Hayo yamebainishwa Leo Februari 23,2025 na Katibu Mkuu Doyo Hassan Doto  wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana  Buguruni Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu huyo amefafanua kwamba kufuatia tamko la Mwenuekiti Taifa wa CHADEMA Tundu Lisu alilolitoa hivi karibuni"No reform,no election",hii ni agenda ya Chadema siyo ya Vyama vya siasa.

"NLD hatujaunga mkono msimamo huo,tutaingia kwenye uchaguzi kwa kuwaeleza wananchi sera kwa ajili ya kupata nafasi mbalimbali za uongozi",amesema Doyo

Aidha ,Doyo amesema vyama vya siasa vipo 19 na vimesajiliwa kwa mujibu WA Sheria kwa hiyo unaposema hakuna uchaguzi wakati lazima utumie njia ya uchaguzi,sisi NLD hatususii uchaguzi.

Pia amefafanua kuhusu mashirikiano ya vyama vya upinzani ili kukikabili Chama cha Mapinduzi Doyo amesema NLD ni mhanga wa mashirikiano.

"Mwaka 2015 Chama cha NLD,CUF,CHADEMA na NCCR Mageuzi viliungana vikiwa na dhamira ya kuing'oa CCM madarakani lakini NLD walidhurumiwa kwa kuwaondoa wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uchaguzi", amesema

Doyo amesema NLD hatujanufaika na Muungano huo wa kisiasa, "ili Muungano uwe mzuri lazima Sheria ya mgawanyo wa haki kwa vyama vya siasa vilivyounga baada ya uchaguziuzingatiwe na uwekwe wazi ili kila chama kinufaike",

Kwa upande wake Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Mfaume Hassan Khamis ameiomba serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwapatia ajira ya kudumu walimu wanaojitolea kwani wanafanya kazi ya kizalendo hivi waangaliwe kwa jicho la kipekee.

Amesema kwamba watanzania waendelee kudumisha amani,utulivu na mshikamano wakati huu tunavyoelekea uchaguzi mkuu tuachane na vyama vya siasa ambavyo vinachochea uvunjifu wa amani nchini

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO