MLAWA AWATAKA VIJANA WILAYANI RUFIJI _ PWANI KUSIMAMIA MAADILI

            Na Eliasa Ally DmNewsOline

                  PWANI 

MDAU  wa Maendeleo Wilaya ya Kilolo, Aidan Mlawa, amewataka vijana kushirikiana na serikali katika kulinda maadili ya jamii na kujikita katika shughuli za ujasiriamali kwa jail ya kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza februari 25,2025  katika Kanisa la KKKT  Usharika wa Ikwiriri, Dayosisi ya Pwani, wilaya ya Rufiji wakati wa uzinduzi wa albamu ya kwaya ya vijana, ya lkwirri Mkoa wa pwani wilaya ya Rufiji Mlawa alichangia shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kununua mashine ya kusaga ili kusaidia kukuza kundi hilo.

Katika mchango wake kwa kanisa, Mlawa pia ameahidi kugharamia ujenzi wa jengo la choo kwa asilimia 75, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya jamii na wadau wa maendeleo katika kuboresha miundombinu ya taasisi za kidini.

Aidha, amewataka vijana kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo imeweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri na kujenga mustakabali wao wa kiuchumi.

"Serikali ina dhamira  ya dhati ya kuhakikisha vijana wanafikia ndoto zao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa,"amesema Mlawa

 Amesema  kuwa yeye si mdau wa maendeleo wa Wilaya ya Kilolo pekee, bali anajitolea kwa maendeleo ya nchi nzima kwa ujumla na ndio ameweza kufanya hivyo nje ya mkoa wa iringa .



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO