CHAMA CHA MAKINI KIMEWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU TUNAPOEKEA UCHAGUZI MKUU
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Chama Cha Makini (Taifa) Coaster Jimmy Kibonde amewataka watanzania kudumisha amani,utulivu na mshikamano tunapoelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na Mwandishi wa DmNewsOnline leo Februari 24,2025 Mwenyekiti wa Chama hicho amesema kuwa dira ya Chama ni kuwahimiza,kuwashawishi na kuwawezesha watanzania kupata Elimu na hasa elimu ya Sayansi na Teknolojia.
Kibonde amesema vyama vya siasa vipo 19 kikiwemo Chama Cha Makini kwahiyo tunawaomba watanzania kukiunga mkono Chama cha makini popote alipo kwa kusikiliza sera za chama hicho kwani kinaongozwa na viongozi makini.
"Sisi Chama Cha Makini tutashiriki kikamilifu uchaguzi na tutasimamisha wagombea wenye sifa kwa nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani Tanzania Bara na Zanzibar",amesema Kibonde.
Ameongeza kuwa wanatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama mwezi Juni kwa ajili ya kupitisha majina ya wagombea wa Urais kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumzia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lisu kuwa "No reform,no election", amesema wao hawaungi mkono kauli hiyo
"Sisi kama Chama cha Makini hiyo kauli ni ya kwao wao kama CHADEMA sisi haituhusu mbaya zaidi hiyo kauli hatuiungi mkono kwa sababu kauli ni dhahiri italeta sitofahamu katika nchi,kuleta vurugu katika nchi ni kauli ambayo kuhatarisha amani na utulivu,ambayo sisi kama Taifa la Tanzania tunajivunia,hata mataifa ya nje wamekua wakizungumzia na kutuone choyo Kwa amani tuliyonayo hivyo hatuiungi mkono na Wala hatutasusia uchaguzi",amesema Kibonde.
Hata hivyo amefafanua kwamba sisi tunawaomba watanzania kutuunga mkono kwa sera za chama tutakazo zitoa kwenye majukwaa.
Kuhusu kauli mbiu ya Chama"Hatulali usingizi,tukilala usingizi nchi itauzwa",
Chama cha Makini kilianzishwa mwaka 2001 wakati huo kikitambulika kama Demokrasia Makini lakini kutokana na mfanano na jina la Chadema waliamua kukaa kikao mwaka 2024 kwa ajili ya kubadilisha jina.
"Agosti 25,2024 Viongozi waliketi kwenye Mkutano na kujadili kubadilisha jina na hatimaye tukaamua kwa pamoja na kuwa na jina la Chama Makini,kwani watanzania wengi walilifananisha na Chama kingine.



Comments
Post a Comment