AIRTEL YATANGAZA PROMOSHENI YA MR.SANTA




Na mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM 

KAMPUNI   ya simu ya Mkononi  Airtel Tanzania katika msimu wa Sikukuu ya Christmass imekuja na zawadi kwa watumiaji wa mtandao huo kupitia promosheni inayoitwa MR. Santa. Mteja na mtumiaji wa mtandao wa Airtel  ili aweze kuingia kwenye kinyang'anyilo cha Mr. Santa anapaswa kufanya  miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea pesa.

Hayo yamebainishwa lDesemba 20,2024  Jijini Dar es Salaam na Meneja mahusiano wa Kampuni hiyo, Jackson Mmbando,  amesema droo ya promosheni hiyo itakuwa ikiwawezesha watumiaji wa mtandao huo kujipatia zawadi kem kem ikiwemo, fedha tasilimu na vitu vya thamani kama luninga, pikipiki , mbuzi , Smart fone za kijanja.

" Hakikisheni wateja wetu wa  Airtel mnafanya miamala wiki hii kwa ajili ya Sikukuu ya Christmass kwa kutuma na kupokea pesa, kulipia bili mbalimbali utaweza kujishindia na kujipatia zawadi kutoka kwa mr. Santa," amesema Mmbando. 


Aidha ameongeza kuwa mtandao wa Airtel unawataka watumiaji wake wakiwemo mawakala, wapenzi kufanya miamala hiyo mara moja kwa wiki hususan siku ya Jumanne ya wiki, ambapo itakuwa inatoa washindi mbalimbali watakuwa waliofanya miamala hiyo.

Ameongeza kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel katika msimu wote huu wa Sikukuu.

“ Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim" amesema Mmbando.

Akielezea jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Mmbando amesema Kwa Wakala wa Airtel anatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha na Kwa mteja anachotakiwa kufanya kununua bando, kulipa bili, kutuma na kutoa fedha, kununua muda wa maongezia au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60# au kupitia 'My Airtel App'.

Kwa upande wake Meneja Huduma Kwa Wateja ,Celina Njuju  amesema Mr. Mazawadi yupo pamoja na watumiaji wa mtandao wa Airtel na unawathamini wateja wake ambapo Mr. Santa atakuwa akizunguka maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha huduma za Airtel zinawafikia wengi ipasavyo.


Hata hivyo droo itakuwa ikichezeshwa mara moja kwa wiki na mshindi atakuwa akipigiwa simu kwa kutumia namba 100 pekee na kuambiwa aina ya zawadi aliyojishindia.


Naye msanii maarufu, Lucas Mhavile," Joti' ambaye ndio amekula shavu la Mr. Santa amesema kuwa msimu huu wa sikukuu Airtel inawajali wateja wake kwa kutoa zawadi Kem Kem kwa kufanya miamala mbalimbali kwa kulipia bili, kutuma na kupokea pesa, nunua cho chote ambapo unajitengenezea nafasi kubwa ya kupata zawadi.



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO