MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI AMETOA UFAFANUZI KUHUSIANA UPOTOSHAJI WA TAKWIMU ZA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 UNAOENDELEA KWA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI HUSUSANI MITANDAO YA KIJAMII




Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM 


 MTAKWIMU Mkuu wa   Serikali Dkt.Albina Chuwa ametoa ufafanuzi kuhusiana na upotoshaji wa Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 unaoendelea kufanyika kwenye baadhi ya vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii.

Hayo ameyabainisha Oktoba 28,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa kwa mujibu wa Kifungu Cha 6 Cha Sheria ya Takwimu SURA 351 kinamtaka Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoa ufafanuzi wa tafsiri sahihi ya takwimu zinazotolewa au zinazopotoshwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Aidha,Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa Kuhusu Takwimu Rasmi(United Nations Fondamental Principles of Official Statistics),Kanuni Na.4 ambayo inaeleza"Ofisi za Takwimu zinahaki na wajibu wa kutoa ufafanuzi juu ya tafsi potofu na matumizi mabaya ya takwimu rasmi".amesema

Dkt.Chuwa amesema kwamba Serikali kupitia Waziti wa Nchi,Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikalo za Mitaa (TAMISEMI).Mhe.Mohamed Mchengerwa Oktoba 20,2024 alitoa taarifa juu ya matokepya zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaautakaofanyika Novemba 27,2024.

Taarifa hiyo ya Serikali ilionesha wananchi waliojiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ni 31,282,331 sawq na asilimia 94.83 ya watu wote wenye umri wa kujiandikisha kwa mwaka 2024.Hata hivyo tangu kutolewa kwa taarifa hiyo kumekuwepo na taarifa za kupotosha takwimu hizo kwenye baadhi ya vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii kwamba takwimu za wananchi walioandikishwa hazina uhalisia na kwamba idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya watu wanaostahili kujiandikisha kupiga kura inayotokana na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Amesisitiza kuwa ifahamike takwimu wanazozungumzia watu hao  ni takwimu zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na kwamba  ulinganishaji wanaoufanya hauendani  na hali halisi ya idadi ya watu wenye sifa za kujiandikisha kupiga kura mwaka 2024.Kwa hesabu za kawaida ni kwamba idadi ya watu nchini kwa mwaka 2022 haiwezi kulingana na idadi ya watu kwa mwaka 2024 kwani hivi sasa tayari miaka miwili kamili imeshapita tangu ilipofanyika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

"Kutokana na makadirio ya idadi ya watiu kwa mwaka 2024,idadi ya watu nchini inakasiriwa kuwa Milioni 66.3(watu 66,278,276) sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 3.2 kwa mwaka kama ilivyopatikana kwenye Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.Makadirio haya kwa Tanzania Bara yanakasiriwa kufikia watu Milioni 64.2 (watu 64,241,822 na kwa Tanzania Zanzibar yanakadiriwa kufikia watu Milioni 2.03 (watu 2,036,454).Kwa makadirio haya ,wananchi tunapaswa kufahamu kuwa idadi ya watu kwa mwaka 2024 haiwezi kiwa sawasawa na Ile ya mwaka 2022",amesema Dkt.Chuwa.

Aliendelea kwa kusema kwamba watu waliokuwa na umri wa miaka 16,17 na 18 kwenye Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 hivi Sasa Wana umri wa miaka 18,19 na 20 ambao idadi yao ni 3,785,036 waliolidhi kigezo cha umri wa kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.Kwa msingi huo,idadi ya watu wenye umri wa kupiga kura ni SAWA na watu wote ambaowqka 2022 walikuwa na umri wa miaka 16 na zaidi ama kwa lugha nyimgine mi wale wote ambao ifikapo tarehe 27 Novemba 2024 watakiwa wametimiza umri wa miaka 18 au zaidi.

Hata hivyo amesema mahesabu hayo yanatokana na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022,makadirio ya idadi hiyo ya watu wenye umri wa kupga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambayo ni watu 32,987,579 ni sahihi na ni rasmi kulingana na Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa Kuhusy Takwimu Rasmi na kama ilivyoripotiwa kwenye taarifa ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais,TAMISEMI.

Dkt.Chuwa ameeleza kuhusu kiwango cha uandiloshaji kwa mikoa,imejitoleza baadhi yake kuwa na asilimia zaidi ya 100 ya wati walioandikishwa.Naomba ifahamike kuwa watu wana tabia ya kuhamahama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine (internal migration).Hivyo uandikishaji wa watu wengi zaidi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwenye baadhi ya mikoa umechangiwa na kiwango cha uhamiaji wa watu kutoka mikoa mingine.

Aliongeza kuwa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ilihesabu watu kulingana na mahali walipolala usiku wa kuamkia ailu ya Sensa yaani tarehe 23 Agosti 2022.Kwa hiyo ,hili ni jambo la kawaida na linalowezekana kutokea kama ilivyotokea katika mikoa hiyo ya Pwani(asilimia  112.61); Tanga(asilimia 110.82); Mwanza(asilimia 106.58); Dodoma (asilimia 104.19); Iringa (asilimia 100.54).Sote tunafahamu kwa mfano; idadi kubwa ya watu mkoa wa Pwani hasa katika wilaya ya Bagamoyo,Kibaha,Kisarawe na Mkuranga.Kwa hiyo ongezeko hili la watu kwenye maeneo hayo linachangiwa ma kuhama kwa watu na SI kwa kuandikisha watu waliokosa sifa.

"Mikoa yenye asilimia ndogo ya uandikishaji ni Ile ambayo chambuzi za litakwimu zinaonesha ni mikoa yenye uhamaji mkubwa wa watu kwenda kwenye majiji",amesema

Dkt.Chuwa ametoa takwimu za Sensa kwa makundi kama ifuatavyo.Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022,idadi ya watoto walio na umri chini ya miaka 15 (under 15) nchini ilikua 26,399,989 sawa na asilimia 42.8; Idadi ya wtu wenye umri wa kufanya kazi wenye umri wa 15 Hadi 64 (Working Age Population) walikuwa 33,000,128 sawa naasilimia 53.4; na idadi ya Wazee (Miaka 65+) walikuwa 2,341,003 saww na asilimia 3.8.Kusema wastani wa watoto chini ya umri wa miaka 15 kuwa ni asilimia 60 Hadi 70 ni upotoshaji mkubwa.Hata lwa viwango vya Afrika,asilia ya watoto ni kati ya 40 hadi 45 na si vinginevyo.

Pia amesisitiza kuwa takwimu rasmi za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351 kwa maana hiyo,taarifa iloyotolewa na Serikali ya Idadi ya wananchi waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Miata utakaofanyika tarehe 27 Novemba,2024 ni sahihi kwa sababu kiujumla idadi ya watu wote waliojiandikisha nchini haijavuka ile inatotokana na matokeo ya  Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.Kwahiyo nitoe Rai kuwa tusipotoshe umma,takwimu hizi hazina mashaka yoyote.Aidha, ni kosakisheria kupotosha umma kwa kutumia takwimu rasmi kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351.

Alimalizia kwa kusema kuwa nawapongeza wananchi wote kwa kuhamasika na kujitokeza kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga Kura kwa kiwango cha asilimia 94.83 ambayo haijawahi kutokea katika zoezi kama hili kwa miaka ya hivi karibuni.Mwitikio huu unatokana na hamasa zilizofanywa na viongozi mbalimbali sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha elimu kwa wananchi kama ilivyooneshwa kwenye matokeo ya Sensa ambapo asilimia 83.0 ya Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika kwa lugha yoyote.Matokeo haya yanashabihiana na mwitikio wa wananchi waliojitokeza na kukubali kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi ya  Mwaka 2022 ambapo asilimia 99.9 ya Watu wote nchini walihesabiwa na ameendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024 kwani ni haki ya kila mmoja wetu kikatiba kwa maendeleo yetu sote.



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO