MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA KANDA YA KASKAZINI YAADHIMISHWA LEO




Na Ahmed Mahmoud,DmNewsOnline
  KILIMANJARO 

SERIKALI imesisitiza kuweka nguvu zaidi kwa wote walioathirika na urahibu wa dawa za kulevya kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwemo kuwarudisha katika maisha ya kawaida na kuwapatia Elimu ya ujasiriamali sanjari na mikopo. 

 kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa kupinga dawa za kulevya nchini inaakisi malengo ya mapambano ya vita dhidi ya dawa za kulevya ili kuikinga Jamii hususani Watoto na vijana wasijihusishe na matumizi Wala biashara haramu dawa.

Hayo yamesemwa na  Mganga  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Charles Mkombachepa akimuawakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga dawa za kulevya Duniani  kwa Kanda ya kaskazini .

Maadhimisho hayo yamefanyika jijini  Arusha kwa ushirikiano na Kanisa la wasabato na DCEA Kanda ya kaskazini yenye kauli mbiu; "wekeza kwenye Kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya".

Mkombachepa amesema kauli hiyo inatoa ujumbe wa kutia nguvu kuikinga Jamii hususani vijana wasijihusishe na matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya pia wale wote waliothirika na matumizi warahibu tuwekeze kuwapatia matibabu ya urahibu wa dawa za kulevya na Elimu ya kuwarudisha katika Maisha.

Kwa Upande wake Afisa Ustawi na Elimu DCEA Kanda kaskazini Sarah Ndaba katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu DCEA Kanda ya kaskazini itaendelea kuratibu shughuli  za kudhibiti na kupambana na tatizo la dawa za kulevya katika Mikoa ya kaskazini Tanga Arusha Kilimanjaro na Manyara  zikiwemo shughuli za kuelimisha na huduma za ustawi wa jamii pamoja na operesheni dhidi ya wahalifu wote wa dawa za kulevya.

Tumeamua kushirikiana na kanisa la wasabato sababu Kuna uhusiano Mkubwa kati ya watu kujihusisha na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya  na kukosa Imani ya mungu na malezi ya kidini tunaamini madhehebu yote yanakataza waumini wao kujihusisha na dawa za kulevya ndio maana tukaamua kuunganisha nguvu kwa sababu ya malezi ikiwa dini zote zinapinga vita dawa za kulevya pia tumetoa Elimu kwa makundi ya watu 300,000 kuanzia juni 2023 hadi Juni 2024.

Naye Mwenyekiti wa SDA Jimbo la kaskazini ameitaka Jamii kumbuka kujali Afya yako kwani Mungu anawakupenda wala usikubali kubomoa Afya yako kwa kufuata vishawishi mbalimbali vinavyoashiria kuharibu Afya yako.

"Jali Afya yako kwa sababu Mungu anawapenda kwa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya tusiharibu Afya zetu kwa kuharibu Afya zetu" Amesema 

Awali akitoa ushuhuda, mmoja wa aliyekuwa muathirika wa dawa hizo fredrick Remmy amesema hapo Awali  hatukuwa na Elimu ya dawa za kulevya ndio maana wengi wetu tulifuata kampani ila kwa Sasa nimekuwa Balozi naenda kutoa elimu kwa wenzangu ila nilipoteza Mali za familia Nyumba ya Mamaangu mzazi nashukuru Kliniki ya Mkuu wa Mkoa inaendelea  kunisaidia kupata haki hiyo hivyo nawahusia vijana wenzangu ogopa sana dawa matumizi ya dawa za kulevya.



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO