CCM KIBAHA MJI YATOA TAMKO LA KULAANI VITENDO VYA MAUAJI YA BODA NA ALBINO



Na Victor Masangu,DmNewsOnline
KIBAHA 

CHAMA cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini (CCM) kimelaani vikali vitendo vya  matukio ya mauaji ya madereva wa boda boda yanayoendelea katika maeneo  mbali mbali.

Akitoa tamko hilo katika kikao cha halmashauri kuu ya chama Mwenyekiti wa (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka alisema kwamba wameamua kwa pamoja kutoa tamko hilo kutoka na kukithiri kwa matukio hayo.

Nyamka amesema kwamba matukio hayo ya unyang'anyi wa kuporwa pikipiki na kufanya mauaji yanafanywa na kikundi cha majambazi.

Amefafanua kuwa hivi karibuni kumetokea tukionla Katibu wa CCM tawi la Miswe kata ya Mbawa ambapo ndugu Sitaki Pazi kuporwa pikipiki na kuuwawa.

Pia Mwenyekiti Nyamka amesema kwamba chama pia kinalaani vikali mauaji ya kikatili aliyofanyiwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino)  Asimwe Novat mwenye umri wa miaka miwili na nusu.

Katika hatua nyingine chama cha mapinduzi kimetoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa hatua ambazo limeanza kuzichukua na kuwatia mbaroni baadhi ya watuhumiwa na kuomba waongeze kasi ili hali hiyo itoweke kabisa nchini.

Pia katika tamko hilo limempomgeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka kwa kuweza kusaidia familia yenye watoto wawili wenye ulemavu wa ngozi(Albino).

Amesema kwamba Mbunge Koka amewasaidia watoto hao wawili kwa kuwavutia huduma ya maji safi na salama kutoka Dawasa pamoja na kuwapatia jiko la gesi.

Nyamka amesema kwamba Mhe.Mbunge ameguswa kwa kuinarisha ulinzi kwa familia zenye uhitaji maalumj na watu wenye ulemavu wa ngozi.

Pia ameongeza kuwa siku zote chama cha mapinduzi kinaubiri amani na utulivu hivyo wanaliomba jeshi la polisi kuebdelea kuimarisha ulinzi kwa wananchi pamoja na mali zao.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka alisema kwamba atahakikisha anaweka mipango ya kuwalinda na kuwatunza watu wenye ulemavu wa ngozi.

Koka amesema kwamba ataendelea kuwasaidia kwa hali na mali watu wenye ulemavu ili waweze kuishi katika mazingira ambayo ni rafiki na katika hali ya ulinzi na usalama.

Aidha Koka ametoa wito kwa wananchi wa Jimbo lake kuwa na umoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola endapo wakibaini watu ambao wanahusika katika matukio ya mauaji.



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO