RAIS DKT.SAMIA ATANGAZA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1,082




Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametanga msamaha kwa Wafungwa 1,082 ambapo Wafungwa 29 kati yao wameachiliwa huru leo Aprili 26, 2024, Wafungwa 20 waliohukumiwa adhabu ya kifo wamebadilishiwa adhabu ya kifo kuwa kifungo cha maisha, Wafungwa 27 waliohukumiwa kifungo cha maisha wamebadilishiwa adhabu kuwa kifungo cha miaka 30 na Wafungwa 1,006 wamepunguziwa adhabu zao na watabaki gerezani na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki. 

Taarifa iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema msamaha huo wa Rais Samia ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania. 

“Ni matarajio ya Serikali kuwa Wafungwa walioachiliwa huru leo watarejea tena katika Jamii kushirikiana na Wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani”

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO