ORYX GESI WAENDELEA KUTIMIZA NDOTO ZA RAIS DKT SAMIA ,WAGAWA MITUNGI YA GESI ARUSHA , WAZIRI JAFO AONGOZA ,GAMBO NAYE ANENA




Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
 ARUSHA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Dk.Selemeni Jafo ameipongeza Kampuni ya Oryx Gas Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.

Dk.Jafo ameyasema hayo leo jijini Arusha katika hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx 1500 pamoja na majiko yake kwa wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini wakiwemo wajasiriamali ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza Oryx kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa Mitungi ya gesi.

"Nina fahamu mpaka leo hii Oryx wameshatoa mitungi ya gesi 32,000 kwa ajili ya jamii na wameshatumia Sh.bilioni 2.7 lakini bado wameendelea kuendelea na kampeni hiyo kwa kutoa mitungi kwa jamii.Oryx wamekuwa mfano mzuri katika kuifikia jamii ,tunaomba na wengine kuiga mfano huu."

Kuhusu madhara ya kutumia nishati chafu, Dk Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne barani Afrika wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na kutumia nishati chafu ikiwemo ya kuni na mkaa.

Hivyo amesema ajenda ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuanzisha kampeni ya kuhamasisha nishati safi Afrika inapaswa kuungwa mkono na watu wote  huku akitumia nafasi hiyo kueleza matumizi ya kuni na mkaa nchini yanasababisha hekta 46242 kupotea kila mwaka kwasababu ya kuni na mkaa.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa na dhamira njema na ndio maana amekuja na kampeni ya nishati safi ya kupikia.Haya ni mapenzi yake na kwasababu tunafahamu nishati chafu inamadhara makubwa katika mazingira.

“Kwanza watu wanalazimika kutegemea kuni na mkaa kwa hiyo kuna uharibifu wa mazingira.Takwimu zinaonesha kila mwaka hekta 46242 zinapotea kwasababu ya kuni na mkaa,”amesema Dk.Jafo.

Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa kina mama na wasichana kwa asilimia kubwa wanatumia wastani wa saa 20 kwa wiki kwa ajili ya kutafuta kuni na mkaa au wakati mwingine ni kinyesi cha wanyama.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman amemetumia nafasi hiyo kuelezea madhara yanayotokana na kutumia kuni na mkaa ambapo amesema nchini  Tanzania, wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na kuni. Kupika na gesi ya Oryx itatatua jambo hili.

Hivyo amesema kupika kwa kutumia gesi ya Oryx huzuia ukataji miti, kwa hiyo husaidia kulinda mazingira huku akieleza pia  kutumia gesi ya Oryx huzuia wanawake kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa msituni.

"Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx ni kupika kwa haraka na kwa ufanisi zaidi; kwa hiyo, wanawake wataanda chakula kwa wakati na wanaume hawatalalamika juu ya kuchelewa kwa chakula kinachosababisha mizogo.

Wakati huo huo Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia kuhamasisha nishati safi ya kupikia wameona ni vema kuendelea kuyagusa makundi mbalimbali katika jimbo hilo.

Amesema kuwa kabla ya kugawa mitungi hiyo 1,500 ya Oryx kwa wana Arusha Mjini, tayari ameshagawa pia mitungi 1400 kwa wajasiriamali huku akisisitiza wataendelea na kuyafikia makundi yote yakiwemo ya watoto wanaolelewa vituo vya ya watoto yatima.

Awali wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini akiwemo Asha Mtumwa na Karim Abdallah wamesema ni jambo la kupongeza kuona  Oryx inawakabidhi mitungi hiyo kwani inaenda kuondoa athari ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa matumizi ya kuni na mkaa ambapo inaathari kuanzia.



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO