KAMPUNI YA ORYX YAWAKUMBUKA VIONGOZI WA DINI KILIMAJARO , YAWAPATIA MITUNGI YA GESI 1000


Na Mwandishi Wetu, DmNewsOnline
KILIMANJARO

KAMPUNI ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond wamekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia 1000 pamoja na majiko yake bure kwa viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali mkoani Kilimanjaro ,lengo likiwa kulihusisha kundi kulinda na kutunza mazingira kwa kutotumia kuni na mkaa.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi iliyofanyika katika Chuo cha Polisi(CCP) mkoani Kilimanjaro, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ambaye alikuwa mgeni rasmi ameeleza kwa kina kuhusu umuhimu wa viongozi wa dini kushiriki katika kuihamasisha jamii kutumia nishati safi ya kupikia.


Amefafanua kuwa viongozi wa dini  ni watu wa thamani sana na  watu wanawathamini na  kuwasikiliza, hivyo  viongozi wetu wa dini wanayo nafasi kubwa ya kushiriki katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupika sambamba na kuendelea kuiambia jamii isiendelee kutumia kuni na mkaa ili kuepuka kuharibu mazingira kwa kukata miti.

 “Tunamatumaini matumaini makubwa na viongozi wa dini na ndio ambao wanaweza kutusaidia kuwaelimisha na kuwaambia wananchi kuhusu kutunza mazingira,”amesema Naibu Waziri Kapinga na kusisitiza watu wengine ambao hawana sura ya kimungu ni ngumu kuaminika kwa jamii.


Amesisitiza kiongozi wa dini akisema msikate miti watu wanaamini huyo ametumwa na Mungu hivyo hawataka  miti huku akifafanua uharibifu wa mazingira unatokana na ukataji miti imessababisha hata mikoa iliyokuwa na mvua nyingi kama mikoa ya nyanda za juu kusini ambazo zilitakiwa mvua kuanza Novemba zinaanza mwishoni mwa Disemba

“Kwanini kwasababu ya matendo yetu wenyewe ya kuharibu mazingira.Kwahiyo tunaamini viongozi wa dini mpo katika nafasi ya kutusaidia kuendelea kukumbusha jamii kwamba dunia hii ambayo tumepewa zawadi na Mwenyezi Mungu ni haki ya kila mmoja kuilinda leo, tunawatoto na wajukuu na tutakuwa na vitukuu pia, sasa kama rasilimali zote tulizonazo tutazichezea leo hawa wajuu na vitukuu vitaishi katika mazingira gani”


Pia amesema kuwa katika kampeni hiyo ya kuhamasisha matumizi ya nishati ya kupikia wamekuwa wakihusisha zaidi wanawake kwasababu wanawake ndio wanaokaa jikoni kupika kuandaa chakula.“Mwaka 2024 tusikubali kupika kwa kuni wala mkaa.“Tunashukuru sana oryx kwa kutupatia majiko ya gesi.”

 Kuhusu kampeni ya nishati safi ya kupikia,amesema mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na  mkutano wa dunia wa mazingira ambapo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alienda na ajenda mahususi ya kumkomboa mwanamke wa Afrika sio mwanamke wa Tanzania peke yake.


 “Kwa hiyo ndgu zangu tunapozungumzia nishati safi ya kupikia tunazungumzia mambo ambayo yamebebwa ndani ya moyo wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ni ajenda yake ambayo yeye mwenyewe ameibeba. Tunapozungumzia wanawake wa Afrika tunazungumzia na wanawake wa Tanzania ,kwa hiyo kwa lugha nyepesi wanawake wa Tanzania ndio wabeba bendera wa kumsaidia Rais kwenye ajenda hii ya nishati safi ya kupikia ili tuwe mfano kwa mataifa mengine,”amesema.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoite Araman ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivunia kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, watoto na wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia.


“Kufanya hivyo tunaamini tunaikomboa jamiina taifa kwa ujumla wake kwani kupika kwa gesi ya Oryx kuna maanisha kuboresha afya za kinamama kwa kueuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa.Pia tunaweza watoto kupata muda wa kwenda shule badala ya kutumwa kutafuta kuni,”amesema Fundi.

Amesisiza kampuni hiyo kwa kutambua nafasi ya viongozi wa dini imeona ni vema sasa ikatoa mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake kwa kundi hilo sambamba na kuelezea kwa kina umuhimu wa kutunza mazingira na wanaamini kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusema na kusikilizwa, hivyo watakapokuwa mabalozi wa kuzungumzia nishati safi ya kupikia jamii itabadilika na hivyo kuokoa mazingira.

Aidha amekumbusha kuwa mwaka 2021 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia na alitoa maono yake ya kwamba ifikapo mwaka 2032  asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi, hivyo kuanzia hapo Oryx iliongeza nguvu na hadi sasa ya mitungi 19000 bure yenye thamani isiyopungua Sh.bilioni 1.5.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO