DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA EREA SEKTA YA NISHATI


Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline         

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Udhibiti wa huduma za Nishati kwa nchi za Afrika Mashariki (EREA) Dkt. Geoffrey Mabea leo tarehe 26 Februari, 2024 jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali ya nishati kwa nchi wanachama na umuhimu wa kujenga uwezo wa Wataalam katika Sekta ya Nishati ili kuongeza tija na huduma bora kwa wananchi.
 

Kikao hicho  kimehudhuriwa na Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar Mhe. Shaib Kaduara na Wataalam kutoka EREA.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO