TABIO NA ENVIROCARE YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MBEGU ZA ASILI



Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline.

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Tanzania Allience  for Biodiversity (TABIO) chini ya uwezeshwaji wa  shirika la Afrikani Biodiversity Network (ABN) na ENVIROCARE  leo Disemba 18, 2023 wameendesha mafunzo Kwa waandishi wa habari wanaondika Habari za kilimo hai Kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu mbegu za asili.

Akizungumza  katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Leo Disemba 18 ,2023 , mkurugenzi na mratibu wa Tabio Abdallah Mkindi Amesema kuwa waandishi wa habari ni watu muhimu sana hivyo wao kama taasisi wameona nimuhimu kuwapa elimu hiyo.

Amesema Kwa kutumia kalamu zao na vyombo vingine vya habari wanauwezo mkubwa wa kuwafikia wadau mbalimbali hasa katika kujua umuhimu wa mbegu za asili 

"Kimsingi mbegu za asili zimetoka katika uasili wake ambao mi polini na wao kama Taasisi kazi yao ni kuziweka kwenye mfumo mzuri ."Amesema 

Kwaupande wake David Manongi mtaalamu wa mbegu tafiti ,uzalishaji na sera kutoka Tabio,Amesema  mafunzo hayo yataendelea kuwajengea uwezo waandishi juu ya  mbegu za asili..






































Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO