RAIS SAMIA AMETOA BILION 755 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOA WA KILIMANJARO NDANI YA MIAKA MIWILI.


Na Mwandishi wetu, DmNewsOnline

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin babu amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani imetoa zaidi ya shingili bilioni 755 katika kipindi cha miaka miwili na nusu fedha zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa huo pekee.

Ameyasema hayo alipo ongoza harambee ya  kuchangia mwendelezo wa ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya Wadventista wasabato jimbo la kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.


Amewaasa waumini na viongozi wa dini hiyo kuendelea kumuunga Mkono na kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta Maendeleo.

"Kwenye mkoa wa Kilimanjaro Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani ametuletea takribani shilingi bilioni 755 kutekeleza miradi mbalimbali kwenye mkoa wa Kilimanjaro ikiwemo  jengo la mionzi Hospital ya KCMC kubiresha huduma ya afya pia jengo la Mama na mtoto Katika hospital ya mawezi pia manunuzi ya vifaa tiba,Mradi mkubwa wa Maji Same, Mwanga -Korogwe, Hospital kubwa ya wilaya ya Same lengo la Mhe.Rais ni kuona wananchi wake wananufaika na huduma pia kupiga hatua kimaendeleo". Alisema Nurdin Babu.

Pia mkuu huyo wa Mkoa amechangia shilingi million 5 na kuwaasa  wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo  muhimu. 


Awali Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni Ameshukuru ushirikiano uliopo  baina yao viongozi wa Dini kwa serikali  akisema imerahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo mipango  ya maendeleo kwenye wilaya ya Same.

"Nisisitize tuendelee kushikamana kutunza amani na upendo tunu ya taifa letu tangu enzi za waasisi wetu, niwaombe pia waumini na viongozi wa Dini kuendelea kumuombea Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani aweze kuifanya vizuri zaidi kazi kubwa ya kujenga Taifa letu". Alisema mkuu huyo wa Wilaya.

Askofu wa kanisani la Waadventista wasabato kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mussa Mzumbi amesema harambee ya ujenzi wa ofisi za Konferensi ni kwa yoyote atakayekuswa kuchangia kwa sababu ni sehemu ya ibada kwa Mungu na kujenga mahusiano mazuri kwa watanzania na ambao sio watanzania.


"Tulipoanza hadi kufikia hatua hii zimetumika Milion 416,484,000 na changizo hili la kuchangia zaidi ya Milion 685 ni kwa ajili ya kuendeleza tunategemea  kukamilisha eneo la Chini na kupandisha nguzo za Ghorofa ya kwanza hadi kupaua". Alisema Askofu  Mussa Mzumbi.

Askofu Mzumbi amemuomba Mkuu wa Mkoa Klimanjaro kumfikishia Salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya waumini wa kanisani la Waadventista wasabato na kuahidi tunaendelea kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo.






Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO