NDUGULILE ATAKA KIGAMBONI IWE DUBAI AU GUANGZHOU YA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, DmNewsOnline

MBUNGE  wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na wana Kigamboni katika Tamasha la #KigamboniPatamu, ameonesha matamanio yake ya kuifanya Kigamboni kuwa Dubai au Guangzhou ya Tanzania.


Dkt Ndugulile amesema kuwa Kigamboni ina ardhi ya kutosha, ukanda wa bahari wenye urefu wa 70km na bandari iliyo karibu na Wilaya hiyo. Hivyo, aliitaka Serikali kufikiria kuiwezesha Kigamboni kuwa kitovu cha utalii na uwekezaji nchini.

Pia amemshukuru Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miradi mingi ambayo anaielekeza Kigamboni na kuifanya kuwa Wilaya inayokua kwa kasi zaidi nchini.


Mgeni Rasmi katika hafla hii, Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Nchemba alisema kuwa amepokea wazo na kwamba wataenda kulichakata ndani ya Serikali.

Tamasha la Kigambonipatamu limeandaliwa na Serikali ya wilaya chini ya Mkuu wa Wilaya Halima Bulembo kwa lengo la kukuza uwekezaji ndani ya Kigamboni

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

MWAKIPOSA ASHINDA NAFASI YA UWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI YA MTAA MKOA WA DAR ES SALAAM

KILINDI BARABARA BADO NI CHANGAMOTO