Posts

TIRA YAWAKUTANISHA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI ,WAJIPANGA BIMA UWE WIMBO WA WATANZANIA WOTE.

Image
    Na Mwamdishi wetu,DmNewsonline                  DODOMA AHADI ya serikali ya kutoa Bima ya Afya kwa wote ikiwa mbioni kuelekea kutimizwa, Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) nayo imeapa kudhibiti soko la bima nchini ili kuimarisha usalama na uchumi wa nchi. Akizungumza kwenye semina ya siku mbili iliyofanyika Novemba 18-19 mwaka huu, katika ukumbi wa mikutano wa jengo la ofisi za Mamlaka hiyo maarufu TIRA BIMA HOUSE lililopo Njedengwa,   Kamishna wa TIRA,  Dkt. Baghayo Saqware amesema hatua hiyo itaondoa kabisa udanganyifu katika soko la bima.  Sambamba na hilo itawajengea ufahamu wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwajibikaji katika sekta ya bima. "Malengo ya semina hii kwenu wahariri, tushirikiane kufikisha elimu ya bima kwa wananchi, hilo likifanyika ipasavyo dhana potofu kuhusu bima zitaisha."amesema  "Wanahabari mkichochea elimu ikaenea kwa watanzania wote, uhitaji wa bima utaongezeka hata ufahamu kw...

PROF.MSOFFE:MILANGO YA UWEKEZAJI WA NISHATI YA SAFI KUPIKIA IKO WAZI KWA WADAU KUWEkEZA

Image
   Na mwandishi wetu,DmNewsOnline                  BRAZIL NAIBU Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa. Peter Msoffe amesema milango ya uwekezaji wa nishati safi ya kupikia ipo wazi kwa wadau wanaotaka kuwekeza.   Amesema hayo ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake na wadau mbalimbali wa masuala ya hifadhi ya mazingira pembezoni mwa Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaofanyika katika Jiji la Belem, Brazil.   Prof. Msoffe akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Burn Manufacturing Bi. Caroline Amollo ambayo inajihusisha na utengenezaji wa majiko ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania amemshukuru na kupongeza kwa shughuli hizo.   Alimuleza mdau huyo kuwa Serikali ya Tanzania inatambua jitihada za wadau wa maendeleo kama kama hao katika kuchangia upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu kwa wananchi kote nc...

BAKARI MACHUMU AWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU

Image
TEUZI 

MABAKI YA MWILI WA MTANZANIA JOSHUA MOLLEL YAWASILI NCHINI TANZANIA

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline MABAKI  ya mwili wa Kijana Joshua Mollel aliyeuwawa nchini Israel na wapiganaji wa HAMAS Oktoba 07, 2023 yamewasili leo Novemba 19, 2025 katika kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA). Mabaki ya mwili huo yamepokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania ukiongozwa na  Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa na Balozi Silima Haji Kombo.  Mabaki ya Kijana Joshua Mollel yanatarajiwa kuzikwa   kesho  Novemba 20,  2025 mtaa wa Njiro, katika kata Orkesumet Wilaya ya Simanjiro,  Mkoani Manyara.   

MANARA:TUJIULIZE TANZANIA IMETOKA WAPI.

Image
   Timothy Marko DmNews online            DAR ES SALAAM  DIWANI  wa kata ya Karikoo Jijini Dar es Salaam Haji  Sunday Manara amewataka Vijana Kudumisha Amani nakusisitiza kuwa  Suala la Amani nikipaumbele cha kwanza katika misingi ya kitaifa. Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam  leo Oktoba 19,2025 Manara amesema enzi ya Miaka ya 1980 Tanzania ilikuwa inapitia Changamoto Ikiwemo ukosefu  wa Chakula Watu walikuwa Wakipanga foleni kwaajili ya unga na Sukali . ,, Nchi hii imepitia wakati mgumu sana, lakini kipindi chote hicho Haki haikudaiwa kwa Maandamano, Changamoto za Ajira ni Changamoto za kidunia ,, Amesema Manara . Manara akisisitiza Suala la Amani utaitwa Chawa lakini ukweli tumekula unga wa njano na kuwa Katika Nchi ya Tanzania hakuna kitu cha kudaiwa isipokuwa Amani. ,, Kabla ya Kuandamana Nilazima tujiulize Mwaka 1980 Tanzania ilikuwaje Mwaka 1987Ndio tulikuwa nasera za kuleta Bidhaa,Hakuna k...

ADA -TADEA YAMVUA UANACHAMA MGOMBEA MWENZA

Image
  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline           Dar es Salaam  KAMATI Kuu ya Chama Cha ADA -TADEA  kimewavua uanachama wanachama wake  kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za chama hicho huku wakijaza nafasi zilizokuwa wazi. Waliovuliwa uanachama ni pamoja na aliyekuwa mgombea mwenza chama hicho, Ali Makame Issa,  Katibu wa  Baraza la Vijana, Alphonce Mayunga na Katibu  Mkoa wa Mwanza, Deusdedit Tiba. Katibu Mkuu wa ADA-TADEA, Salehe Msumari amesema hayo  leo  Novemba19,2025 Jijini Dar es Salaam  wakati akizungumza na vyombo vya habari na kuongeza kuwa  baada ya chama kujaza nafasi za viongozi hao watapeleka taarifa kwa  Msajili wa Vyama vya Siasa. Aidha,amesema wagombea hao wamevuliwa uanachama kwa sababu mbalimbali na kwamba kuanzia sasa matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyekuwa mgombea mwenza hayatatambuliwa na chama hicho. Pia ameeleza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti  Zanzibar imechukuliwa...

ADAKWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJITEKA

Image
     Na Allan Kitwe,DmNewsonline                     TABORA  JESHI la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia Hadija Jimmy Mrijo (39) mpare, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na watu wasiojulikana ili ajipatie fedha isivyo halali kutoka kwa mume wake. Kamanda wa Polisi Mkoani hapa SACP Richard Abwao amethibitisha kushikiliwa mwanamke huyo ambaye ni mke wa Emanuel Peter Charles mkazi wa Tabora Mjini. Amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa mumewe kuwa alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akidai kuwa wamemteka hivyo awatumie fedha kiasi cha sh mil 2 ili wamwachie. Amedokeza kuwa mume wa mtuhumiwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kusikia mlio wa kuteswa aliingiwa na hofu na kuanza kutafuta kiasi hicho cha fedha ambapo alifanikiwa kutuma kiasi cha sh 1,385,800/-. Kamanda Abwao amefafanua kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina tumebaini kuwa mtuhumiwa hakuwa ametekwa ila alijiteka mw...