PROF.MSOFFE:MILANGO YA UWEKEZAJI WA NISHATI YA SAFI KUPIKIA IKO WAZI KWA WADAU KUWEkEZA

   Na mwandishi wetu,DmNewsOnline

                 BRAZIL


NAIBU Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa. Peter Msoffe amesema milango ya uwekezaji wa nishati safi ya kupikia ipo wazi kwa wadau wanaotaka kuwekeza.
 
Amesema hayo ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake na wadau mbalimbali wa masuala ya hifadhi ya mazingira pembezoni mwa Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaofanyika katika Jiji la Belem, Brazil.
 
Prof. Msoffe akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Burn Manufacturing Bi. Caroline Amollo ambayo inajihusisha na utengenezaji wa majiko ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania amemshukuru na kupongeza kwa shughuli hizo.
 
Alimuleza mdau huyo kuwa Serikali ya Tanzania inatambua jitihada za wadau wa maendeleo kama kama hao katika kuchangia upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu kwa wananchi kote nchini.
 
“Sote tunapaswa kutambua kuwa nishati safi si tu gesi kama ambavyo watu wengi wanafikiri lakini ni njia yoyote ile ambayo unaweza kuitumia katika kuivisha chakula ili mradi usiharibu mazingira kwa kukata miti ovyo,” amesema. 
 
Kwa upande wake  Caroline ameshukuru Serikali kwa kutambua mchango wadau hususan wanaounga mkono juhudi za kukabiliana na changamoto za mazingira kutokana na ukataji wa miti.
 
Alisema ataendelea kufanya uzalishaji wa majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia na kuwafikia wananchi wengi kwa wakati na kwa gharama nafuu hivyo kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kupikia na wakati huo kuiacha misitu bila kuikata. 
 
Ikumbukwe kuwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuchagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kulinda afya na mazingira kwa kuhifadhi miti badala ya kuikata kwa ajili ya kuni na mkaa.   

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.