MLAWA AWATAKA VIJANA WILAYANI RUFIJI _ PWANI KUSIMAMIA MAADILI
Na Eliasa Ally DmNewsOline PWANI MDAU wa Maendeleo Wilaya ya Kilolo, Aidan Mlawa, amewataka vijana kushirikiana na serikali katika kulinda maadili ya jamii na kujikita katika shughuli za ujasiriamali kwa jail ya kujikwamua kiuchumi. Akizungumza februari 25,2025 katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ikwiriri, Dayosisi ya Pwani, wilaya ya Rufiji wakati wa uzinduzi wa albamu ya kwaya ya vijana, ya lkwirri Mkoa wa pwani wilaya ya Rufiji Mlawa alichangia shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kununua mashine ya kusaga ili kusaidia kukuza kundi hilo. Katika mchango wake kwa kanisa, Mlawa pia ameahidi kugharamia ujenzi wa jengo la choo kwa asilimia 75, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya jamii na wadau wa maendeleo katika kuboresha miundombinu ya taasisi za kidini. Aidha, amewataka vijana kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu...