KAMPUNI YA ORYX YAWAKUMBUKA VIONGOZI WA DINI KILIMAJARO , YAWAPATIA MITUNGI YA GESI 1000
Na Mwandishi Wetu, DmNewsOnline KILIMANJARO KAMPUNI ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond wamekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia 1000 pamoja na majiko yake bure kwa viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali mkoani Kilimanjaro ,lengo likiwa kulihusisha kundi kulinda na kutunza mazingira kwa kutotumia kuni na mkaa. Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi iliyofanyika katika Chuo cha Polisi(CCP) mkoani Kilimanjaro, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ambaye alikuwa mgeni rasmi ameeleza kwa kina kuhusu umuhimu wa viongozi wa dini kushiriki katika kuihamasisha jamii kutumia nishati safi ya kupikia. Amefafanua kuwa viongozi wa dini ni watu wa thamani sana na watu wanawathamini na kuwasikiliza, hivyo viongozi wetu wa dini wanayo nafasi kubwa ya kushiriki katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupika sambamba na kuendelea kuiambia jamii isiendelee kutumia k...