Posts

COMPASSION YAFADHILI WATOTO ZAIDI YA 115000 KUPATA ELIMU NA KUWAKOMBOA NA UMASIKINI

Image
Na Benny Kingson,DmNewsOnline  TABORA. ZAIDI ya watoto 115,000 wamefadhiliwa na shirika la maendeleo ya huduma ya mtoto na kijana  nchini COMPASSION  (CIT)kupata elimu ya dini,jamii na kukombolewa kiuchumi ambao wametoka katika familia zenye hali duni ya maisha. Naibu Waziri  Mkuu na Waziri wa nishati Dkt.Dotto Biteko akiwakilishwa na Naibu  Waziri wa afya Dkt.Godwin Mollel  katika kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya COMPASSION kitafa Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye uwanja wa chipukizi mjini humo alihimiza wazazi,walezi na jamii kujitolea kuwasaidia  watoto na vijana kupata malezi bora badala ya kuchangia fedha nyingi  za  harusi na misiba. Biteko alisema kuwa shirika hilo limefankisha kujenga vituo vingi vya kujifunzia watoto na vijana na kuwapatia ujuzi wenye kupatia vipato vya halali na kujihakikishia maendeleo yao na ya familia zao pamoja na ya taifa ambapo wamewezesha kuokoa fedha zilizokuwa zitumiwe na serikali kuvijenga na  s...

ORYX GESI WAENDELEA KUTIMIZA NDOTO ZA RAIS DKT SAMIA ,WAGAWA MITUNGI YA GESI ARUSHA , WAZIRI JAFO AONGOZA ,GAMBO NAYE ANENA

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  ARUSHA WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Dk.Selemeni Jafo ameipongeza Kampuni ya Oryx Gas Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini. Dk.Jafo ameyasema hayo leo jijini Arusha katika hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx 1500 pamoja na majiko yake kwa wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini wakiwemo wajasiriamali ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza Oryx kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa Mitungi ya gesi. "Nina fahamu mpaka leo hii Oryx wameshatoa mitungi ya gesi 32,000 kwa ajili ya jamii na wameshatumia Sh.bilioni 2.7 lakini bado wameendelea kuendelea na kampeni hiyo kwa kutoa mitungi kwa jamii.Oryx wamekuwa mfano mzuri katika kuifikia jamii ,tunaomba na wengine kuiga mfano huu." Kuhusu madhara ya kutumia nishati chafu, Dk Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne barani Afrika wanapoteza maisha kila mwaka k...

DC SAME AAGIZA KUSAKWA KWA WATUHUMIWA WATATU WA MAUAJI YA MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA KAPIMBI.

Image
Na Ashrack Miraji,DmNewsOnline KILIMANJARO MKUU wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ameagiza Polisi kufanya msako na kuwakamata watu watatu wa familia moja wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la mauaji ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Kampimbi kata ya Ndungu, Charles Johnson Mkuruto(58).  Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, mnamo Aprili 26 mwaka huu majira ya saa tano na nusu asubuhi huko kitongoji cha Kampimbi kijiji cha Ndungu kata ya Ndungu mtu mmoja aitwae Johnson Mkuruto(58) Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sinangoa 'A' aliuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani na nyuma ya bega la kulia.  Amesema kuwa, Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Ardhi kata ya Ndungu alikatwa na watu watatu ambao aliwataja kwa majina kuwa ni Mohamad Makundi, Hamad Makundi na Mnandi Makundi na kutoweka kusikojulikana.  Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa, sababu ya mauaji hayo ni mgogoro wa Ardhi uliopo Mahakama ya Ardhi ya Ndungu. "Baraza la Ardhi jana...

CCM TABORA YAANZA KUSIKILIZA KERO ‘LIVE’ NA KUZITATUA

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline TABORA CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tabora Mjini kimeanza kusikiliza na kutatua kero za wananchi papo hapo kwa kutumia Wataalamu wa Mipango Miji, Kamishna wa Ardhi na Maafisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa Tabora. Akizungumzia kabla ya kuanza zoezi hilo jana Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini Mohamed Katete alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho kimepewa dhamana na wananchi kushika dola hivyo kinapaswa kuhakikisha kero zao zote zinasikilizwa na kutatiliwa haraka iwezekanavyo. Amesema kuwa CCM kupitia ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kiliahidi kuwa serikali yake itaboresha maisha ya wananchi na kero zinazowakabili zitatatuliwa, hivyo zoezi hilo ni sehemu ya utekelezaji ilani ya uchaguzi.   ‘Kila mwananchi mwenye kero ya aina yoyote ile aje Ofisi ya Chama, tutamsikiliza na kutoa maelekezo kwa Wataalamu wetu walioajiriwa na serikali ya CCM ili wayafanyie kazi haraka iwezekanavyo, zoezi hili ni endelevu’, amesema. Katibu wa CCM...

MAKONDA AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAANDALIZI YA MEI MOSI KITAIFA

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani (Mei mosi) inayotarajiwa kufanyika kitaifa Mei 01.2024 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha Makonda ametoa wito huo leo, Jumamosi Aprili 27.2024 alipokuwa kwenye kikao kazi cha maandalizi kuelekea siku ya wafanyakazi Duniani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo amesema uwepo wa shughuli hiyo ya kitaifa mkoani humo ni fursa kubwa kwa wakazi wake, na kwamba katika kuchangamkia fursa hiyo uongozi wa mkoa huo umeandaa eneo maalumu (Barabara) kando ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya kutumiwa na wajasiriamali mbalimbali kufanya biashara zao Amesema uwepo wa siku hiyo (Mei mosi) unaashiria uhuru na haki za wafanyakazi mahala pa kazi hivyo ni vyema wananchi wakatambua kuwa ushiriki wao utawaongezea morali watumishi katika kuihudum...

MENEJIMENTI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA TABORA MATATANI

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline TABORA  NAIBU Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete) na kukutana na watumishi ili kupokea taarifa na kusikiliza kero zao. Katika mkutano huo baadhi ya Watumishi wameeleza kukabiliwa na matatizo mengi ambayo hayajashughulikiwa na Menejimenti kwa muda mrefu licha ya Hospitali hiyo kuingiza mapato kila mwezi, na kueleza kuwa hili linawavunja moyo. Wametaja baadhi ya kero hizo kuwa ni kutolipwa stahiki zao kwa muda mrefu ikiwemo fedha za likizo, matibabu, kutopandishwa vyeo na marupurupu mengine ya kiutendaji. Aidha wamelalamikia hali ya mazingira ya hospitali hiyo kutoridhisha hususani katika wodi ya wazazi na maeneo mengine licha ya kuwepo Kampuni iliyopewa kandarasi ya kufanya usafi katika hospitali hiyo. Baadhi ya watumishi wamemweleza Naibu Waziri kuwa Kampuni hiyo haina uwezo wa kazi waliyopewa na kudai kuwa wahusika wanakumbatiwa na Uongozi, kwani licha ya kulalamikiwa hakuna...

RAIS DKT.SAMIA ATANGAZA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1,082

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametanga msamaha kwa Wafungwa 1,082 ambapo Wafungwa 29 kati yao wameachiliwa huru leo Aprili 26, 2024, Wafungwa 20 waliohukumiwa adhabu ya kifo wamebadilishiwa adhabu ya kifo kuwa kifungo cha maisha, Wafungwa 27 waliohukumiwa kifungo cha maisha wamebadilishiwa adhabu kuwa kifungo cha miaka 30 na Wafungwa 1,006 wamepunguziwa adhabu zao na watabaki gerezani na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.  Taarifa iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema msamaha huo wa Rais Samia ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.  “Ni matarajio ya Serikali kuwa Wafungwa walioachiliwa huru leo watarejea tena katika Jamii kushirikiana na Wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani”