KOKA AWASHUKURU VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM KWA USHIRIKIANO
Na Victor Masangu,DmNewsOnline KIBAHA MBUNGE wa Jimbo Kibaha mjini Silvestry Koka kwa dhati wanachama wa ccm pamoja na wananchi wa Kata ya Pangani kwa kuweza kumchagua Yohana Gunze kuwa diwani wa Kata ya Msangani katika uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni. Koka ameyasema hayo machi 26 ,2024 wakati wa kikao mà alunu cha Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji chenye lengo la kujadili agenda mbali mbali kimaendeleo pamoja na kujiandaa na chaguzi mbali mbali ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Amesema Koka aliwapongeza viongozi mbali mbali kuanzia ngazi zote za chini hadi ngazi za juu kwa ushirikiano wao wa dhati katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi wa udiwani hadi uchaguzi mwenyewe. Koka amesema kwamba amefarijika sana kuona wanachama na wananchi kukiamini chama cha mapinduzi na kumchagua kwa kishindo mgombea udiwani wa kata ya Msangani kwa kushinda kwa kishindo kwa asilimia 99.20 "N...