TMA:JUNI HADI AGOSTI KUTAKUWA NA VIPINDI VYA BARIDI.
Timothy Marko DmNews Online
DAR ES SALAAM.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Nchini Tanzania (TMA) imewatadharisha Wananchi kuwa kutakuwa na Hali ya Baridi kwa kipindi cha Mwezi juni hadi Agosti mwaka huu.
Akizungumza Leo Mei 25,2026 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Dkt.Ladislaus Chang'a amesema kuwa hali hiyo ya baridi itaambatana na Upepo mkali katika baadhi ya Maeneo ya nchi .
"Mwelekeo wa Joto,hali ya baridi ya Wastani inatarajiwa katika Maeneo ya ziwa Victoria na kanda ya kusini ya nyanda za juu kusini, Nyanda za juu kusini ikijumuisha Mikoa ya Singida"Amesema Dkt.Chang'a
Dkt.Chang'a Ameongeza kuwa hali ya Joto kiasi na baridi ya wastani inatarajiwa kuikumba mikoa ya ukanda wa Pwani na Maeneo ya kaskazini sambamba na Maeneo ya Nchi kavu.
Amesisitiza kuwa Maeneo ya Nyanda za juu kaskazini ukanda wa Pwani kunatarajiwa kuwa na Baridi ya Wastani.
"Vipindi vya Baridi vinatarajiwa kujitokeza zaidi katika mwezi Julai na
Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko katika kipindi hicho. 







Comments
Post a Comment