MWENYEKITI WA SHIVYAWATA MATEMBA KUFUNGA NDOA JUNI 27,2026,ANAOMBA MCHANGO
Na Mwandiahi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Dar es Salaam (SHIVYAWATA),Charles Matemba anatarajiwa kufunga ndoa na Fatuma Ally Makame Juni 27,2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Wanandoa hawa watarajiwa ni watu wenye ulemavu wameamua kuwa pamoja katika maisha yao ya ndoa jambo ambalo ni jema .
"Tumeamua kufunga ndoa sisi wenye ulemavu kwani watu wenye ulemavu wana moyo wakupenda na hisia kama watu wengine"amesema Matemba.
Bwana harusi Mtarajiwa Charles Matemba akizungumza na waandishi wa habari Mei 17,2026 katika kikao cha kamati ya maandalizi ya harusi yao Bwana harusi mtarajiwa Charles Matemba amesema ameguswa kumuoa Fatuma mlemavu mwenzake kwani wenye ulemavu wamekuwa katika mazingira ya kunyanyapaliwa kutokana na ulemavu walionao kwamba hawawezi kuolewa ama kuoa
Aidha, Matemba ametumia nafasi hiyo kuwaomba ndugu, jamaa, marafiki na wadau mbalimbali kumshika mkono kwa hali na mali ili kufanikisha tukio hilo ambalo muda wake umebaki mchache.
Kwa mtu yeyote ambaye atakuwa tayari kumchangia atume mchango wake kwa namba ya Tigo Pesa-0676701819 na MPESA -0766101802 Jina Charles Matemba ili kufanikisha shughuli hii tunaomba mchango wako kwa kuwa mahitaji ni mengi na bado hakuna kitu chochote kilichofanyoka.
Kwa upande wake Bibi harusi mtarajiwa Fatuma Ally Makame amesema ameamua kufunga ndoa na mlemavu mwenzake kwa kuwa mtu mwenye ulemavu ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine na anahisia kama mtu mzima naye ana moyo wa kupenda kama mtu mwingine.
"Nimeamua kuoana na Bwana Matemba kwani ninaamini kuwa tunasaidiana katika shida na raha na wakati wa sasa watu wenye ulemavu wanajitambua na sio tegemezi kwa kuwa tunawashinda watu wazima kwani tunafanya majukumu yetu na tunajitoaa na kujielewa", amesema Fatuma
Watarajiwa hao wametoa wito kwa jamii kuwa wenye ulemavu wasikate tamaa kwani wanaweza na wasimdharau mtu kwa muonekano wake
Naye Mjumbe wa kamati ya maandalizi Vaileth Samson Mwazembe amesema ameomba jamii kuwaunga mkono maharusi hao watarajiwa kutoka kundi lenye uhitaji maalum kwa chochote ili kufanikisha kwani wanaonyesha mshikamano na mfano katika jamii.
"Nawaomba jamii kuwa begakwa bega na maharusi hawa watarajiwa kwa kuchangia chochote kile ili kufanikisha jambo hili la baraka ",amesema Mjumbe Vaileth

Comments
Post a Comment