AHADI ZA CHAMA CHA MAKINI ZATIKISA ISIMANI WANANCHI KUPEWA MATREKITA 2 BURE KILA KATA
Na Eliasa Ally,DmNewsonline
IRINGA.
ZIKIWA zmesalia siku tatu kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ismani kufutia kifo Cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo William lukuvi kufariki Dunia ,vyamba mbalimbali vimeendelea kunadi sera zake kwa wananchi.
Katika kuhakikisha Chama Chama cha MAKINI kimedhamiria kuchukua kikoba hiyo kimetoa ahadi kwa wananchi kuwa endapo kinampa kura Mbunge wao basi Kila kata ndani ya Jimbo hilo watapewa Trekta kwa ajili ya kilimo bure.
Pia mgombea huyo amesema mbali na kutoa Trekta hizo lakini wananchi wataendelea kunufaika na suala la elimu bure kwa watoto wa familia za kawaida.
Kauli hizo zilitolewa Mei 28, 2026 Katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Mlowa, Kata ya Mlowa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Costa Kibonde, ambapo wananchi walijitokeza kusikiliza sera za Chama hicho.
"Chama chetu kupitia mgombea wetu huyu mkitupa ridhaa katika Jimbo hilo tu tatoa matrekta mawili kwa kila kata ndani ya Jimbo hili ili kuongeza tija ya kilimo na kuwaondolea wakulima adha ya kutumia jembe la mkono."amesema Mwenyekiti Kibonde
Amesema matrekta hayo tayari yametolewa kutoka Denmark na wananchi hawatalazimika kutoa fedha yoyote wakati wa huduma ya kulimiwa mashamba yao, jambo lililozua shangwe na matumaini mapya kwa wakazi wengi wa eneo hilo wanaotegemea kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi.
Katika upande mwingine kauli hiyo imeibua tafakuri kubwa kwa wananchi wengi wanaoamini kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana bila kuwekeza kwanza katika uzalishaji wa chakula na kuinua kipato cha mkulima wa kawaida anayepambana kila msimu kuhakikisha familia yake inaishi.
Licha ya Kuzungumzia sekta ya kilimo viongozi wa Chama hicho Cha MAKINI walieleza kuwa ushindi wao utafungua ukurasa mpya wa maendeleo ya viwanda ambapo kiwanda kikubwa kinatarajiwa kujengwa Isimani kwa lengo la kuzalisha ajira kwa vijana pamoja na kuchochea ukuaji wa biashara ndogo ndogo.
Naye Ofisa wa Uchaguzi wa Chama hicho, Sharifa Suleiman, ametangaza mpango wa kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi Sekondari na kwamba elimu ni haki ya msingi na siyo mzigo kwa wazazi wenye kipato cha chini.
Sharifa amesema pamoja na elimu bure, Chama hicho kitapambana na changamoto ya huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya katika kila kata ili wananchi waache kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu.
Kwa upande wake Mgombea ubunge wa Jimbo la Isimani kupitia Chama Cha MAKINI, Farida Mwaipungu, amesema dhamira yake ni kuendeleza miradi ya maendeleo iliyoanzishwa awali huku akiahidi kuboresha mikopo kwa wananchi pamoja na kuweka mazingira bora ya kiuchumi kwa vijana na wanawake.
Farida pia amtoa ahidi kwa vijana wa bodaboda kuwawezesha kwa mfumo wa mikopo ya pikipiki isio na riba, sambamba na kuanzisha bima ya afya ya “Farida Care” itakayolenga kuwasaidia wakazi wa jimbo hilo kupata huduma za afya kwa urahisi zaidi.
Akihitimisha mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chama cha MAKINI, Ameir Hassan, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura huku akisisitiza umuhimu wa amani, utulivu na mshikamano wakati wa zoezi la upigaji kura. 



Comments
Post a Comment