TPSF YAIOMBA SERIKALI KUJADILI MABADILIKO YA KISERA YA KIKODI.
Timothy Marko DmNews Online.
DAR ES SALAAM
TAASISI ya Sekta Binafsi Nchini Tanzania (TPSF)imeomba Wizara ya Fedha kuweza kukaa na taasisi hiyo ili kuweza kufanya mapitio ya sera ya kodi ilikuweza kuchochea Mazingira Wezeshi ya ufanyaji Biashara.
Akizungumza Leo Febuari 27,2026 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Taasi hiyo Mwanahamis Hussein amesema kuwa lengo kubwa la kutaka kukutana na Wizara ya Fedha ni pamoja na kujadilianaSera mbalimbali za kifedha.
"Tunataka kupeleka Mapitio haya sera kabla ya Bunge la Bajeti"Amesema Mkurugenzi wa Sera na Utafiti TPSF Mwanahamis Hussein.
Mwahamis Ameongeza kuwa lengo nikutaka Mabadiliko ya Sera za kodi katika sekta ya Viwanda na Madini ili kuweza kuchochea Uchumi Nchini.
Amesisitiza kuwa Kikao hicho kitatoa Dira na mwelekeo wa hali ya ukuaji wa Biashara Nchini na kuweza kuchangia pato la taifa.

Comments
Post a Comment