NSVINGA AIPONGEZA SEKTA YA MADINI
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa Kampuni ya Nation Laboratory,Happiness Nsvinga ameipongeza sekta ya Madini kwa kufanikisha makubaliano na Benki ya CRDB kwa lengo la kuwawezeaha wachimbaji kupata mitaji kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.
Akizungumza kuhusu makubaliano hayo,Nsvinga amesema upatikanaji wa mtaji umekuwa changamoto kubwa kwa wachimbaji wengi,hasa wadogo,na kwamba kufanya biashara ya madini jambo gumu.Ameeleza kuwa hatua hiyo inafungua ukurasa mpya kwa wachimbaji kwa kuwawezesha kupata fedha zitakazowaongezea uwezo wa uzalishaji wa kukuza biashara zao.
Amesisitiza kuwa kwa pamoja na umuhimu wa mtaji na maarifa,kipengele muhimu zaidi katika biashara ya madini ni kufanya vipimo sahihi vya madini.
Amesema bila vipimo ya uhakika hata kama mfanyabiashara na mtaji na uzoefu atakosa mwelekeo sahihi.
Nsvinga amewahimiza wadau wote wa biashara ya madini kuhakikisha wanafanya vipimo katika maabara zenye ithibati ya kimataifa ili kupata majibu ya uhakika yatayowaongoza katika kufanya maamuzi sahihi ya uwezeshaji na kukuza sekta ya madini nchini. 






Comments
Post a Comment