MIRADI YA HALMASHURI YA JIJI LA DAR IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 89_Dc MPOGOLO

  Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

           DAR ES SALAAM 

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambapo taarifa hiyo imejikita katika kipindi cha miaka minne ya Julai mpaka Desemba 2025.

Akiwasilisha taarifa hiyo Leo Februari 25,2026 Jijini Dar es Salaam DC Mpogolo amesema taarifa hiyo imejikita katika kipindi Cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na tunamshukuru Rais kwa kutoa fedha nyingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam .

Aidha amesema miradi mingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekamilika kwa asilimia 89.

DC Mpogolo ameeleza kuwa katika Wilaya ya Ilala ina wanafunzi zaidi ya laki nne kwa shule ya msingi na Sekondari na changamoto kubwa ni vyumba vya madarasa lakini Halmashauri imejikita katika upatikanaji wa vyumba na kuhakikisha inajenga  vyumba kwa ajili ya wanafunzi kwa elimu msingi na elimu sekondari pamoja na madawati na jumla ya milioni 400  zimetengwa kwa ajili ya utengengenezaji wa madawati.

Katika bajeti ya mwaka 2026/2027 Halmashauri imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ili kumaliza changamoto ya upatika anaji wa  madawati lakini pia changamoto ya vyumba vya madarasa .

Hata hivyo amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia kupokea wana funzi wengi mwaka 2028 zaidi ya wanafunzi 65,000 kutokana na mabadiliko ya mfumo wa elimu na tunatarajia idadi kubwa ya watoto wengi  kuanza kidato cha kwanza hivyo Halmashauri imeendelea kuweka jitihada za dhati kuhakikisha inajenga Madarasa na madawati yatakayoweza kupokea watoto 65,000.

DC Mpogolo ametoa wito kwa wananchi wa Halmashauri kuendelea kushirikiana kwa pamoja kwa watendaji lakini pamoja na wananchi wanapopata changamoto zozote za migogoro mbalimbali wasisite kutoa tarifa na kufika kwenye ofisi za Halmashauri.

Aliendelea kwa kuvishukuru vyombo mbalimbali vya Habari kwa kuendelea kutoa habari  njema  za kazi kubwa zilizofanyika katika Halmashauri na kuwashukuru waandishi wa habari kwa kazi kubwa ambayo wamefanya na kuendelea kushirikiana

Pia amewapongeza wajumbe wa Halmashauri kuu Wilaya ya Ilala wakiongozwa na madiwani na Wabunge kwa  kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi.

Ameongeza kuwa hivi karibuni Wilaya ya Ilala inatarajia kutoa vitambilisho vya kazi kwa Wenyeviti wa Serikali za mitaa wapatao 159  hivi amewataka wavute subira zoezi likikamilika watapatiwa.

Kwa upande wake  Meya wa Halmasgauri ya Jiji la Dar es Salaam Nurudini Sheta ameomba wajumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya waweze kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kufanya kazi kwa weledi na amesema gharama za mafunzo hayo atagharimia yeye.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.