JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA POLISI KUFICHUA UHALIFU.
Na Eliasa Ally,DmNewsonline
IRINGA
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, ameitaka jamii kuacha tabia ya kuficha wahalifu na badala yake kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.
Kamanda Bukumbi ametoa wito huo Februari 27, 2026 akisisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni nguzo muhimu katika kupambana na vitendo vya uhalifu na kudumisha usalama wa jamii.
Aidha, Kamanda Bukumbi anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara kesho Februari 28, katika uwanja wa Shule ya Msingi Mawelewele, Kata ya Mwangata.
Lengo la mkutano huo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya uhalifu pamoja na kusikiliza changamoto zao ili kuimarisha usalama na ulinzi wa raia na mali zao.
Jamii inahimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mkutano huo muhimu.

Comments
Post a Comment