SERIKALI IMEFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWA VIJANA KATIKA UONGOZI WA RAIS SAMIA



Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

               Dar es Salaam 

MRATIBU wa Taasisi ya Together for Samia Gulatone Masiga amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan serikali imefanya mageuzi makubwa ya kuwanufaisha vijana wa Kitanzania katika sekta za ajira,ujuzi na elimu pamojana uwezeshaji wa kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Januari 26,2026 Jijini Dar es Salaam wakati wa kumbukizi ya maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Samia yaliyoandaliwa na taasisi ya Together for Samia,amesema  Rais ametoa fursa nyingi kwa   vijana zenye mafanikio.

Aidha amesema kwamba Rais Samia amewekeza kwa vijana katika kizazi cha Sasa na kijacho hasa katika ujenzi wa vyuo vya ufundi na ujuzi katika wilaya zaidi 62 nchini jambo lilopelekea vijana kupata fursa ya kujiajiiri na kushinda katika soko la ajira.

Aliendelea kwamba Rais Samia amewekeza kwa vitendo,kwani vyuo ni chachu ya kuwaapatia vijana ujuzi unaohitajika katika maisha ya Sasa na baadae.

"Rais Samia amefanya mageuzi  makubwa katika sekta ya elimu kwa kuja na mtaala mpya unaaolenga kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari wanakuwa na maarifa na stadi zitakazowawezesha kujiajiri na kujikwamua kiuchumi

Aliongeza kwamba Rais amewekeza katika sekta ya Nishati safi hatua inayochochea maendeleleo ya viwanda na biashara kwa kuwainua vijana waweze kujiajiiri na kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wa Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana Innovations,Dorcas Mshiu amesema ameungana na Watanzania kuadhimisha siku ya kumbikizi ya kuzaliwa Rais Samia kwa kutambua mchango wake wa kufungua fursa  kwa vijana.

Mshiu amesema kupitia Wizara ya Viwanda na biashara vijana wengi wamesajili biashara zao kutokana na mazingira kuwa rafiki nchini na mipaka ya uwekezaji ndani na nje imekuwa rafiki kiuwekezaji.

Mkurugenzi Dorcas amesema Rais ameweka mpango mkakati maalum wa mikopo yenye riba ya asilimia 4 kwa vijana na umekuwa msaada mkubwa kwa vijana

Naye Mshiriki  Nathaniel Samson  amewaomba watanzania kumuombea  Rais Samia kwani akiahidi jambo lolote lile yeye anatekeleza kwa vitendo   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.