MWENYEKITI TUME HURU YA UCHAGUZI AWATAKA WARATIBU NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUZINGATIA SHERIA.

    Na Eliasa Ally,DmNewsonline

              IRINGA 

MWENYEKITI  wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi   Jaji  Jacob Mwambegele amewakumbusha wasimamizi na waratibu wa uchaguzi kuzingatia weredi Sheria na kanuni za uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha sita ibara ya kwanza na utendaji kazi kwa kuzingatia uzoefu wao bila kupendelea

Jaji Mwambegele ameyabainisha hayo wakati wa ufunguzi  wa mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi ngazi ya mkoa Jimbo na kata yanayofanyika mkoani Iringa kwa siku tatu katika ukumbi wa mkuu wa mkoa  wa Iringa

Mafunzo hayo yanahusisha  waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya  jimbo na kata maafisa uchaguzi,maafisa ununuzi na uhasibu kwa lengo la kukumbushana masuala muhimu kuhusu usimamizi uratibu na uendeshaji mdogo wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Peramiho na udiwani katika kata ya shiwinga.

Pia amewasisitiza  kuheshimu viapo vyao kwa nafasi walizoteuliwa kutekeleza majukumu  yao Kwa kuzingatia katiba ya nchi ,sheria za uchaguzi na kanuni zake kanuni za maadili ya uchaguzi pamoja na maelekezo yanayotolewa na tume katika kipindi cha uchaguzi.

Mbali na hayo Mh.Mwambegele  amewataka wasimamizi na maafisa hao  ambao wanauzoefu  katika uendeshaji wa uchaguzi kuhakikisha wanazingatia maelekezo waliyopewa na tume   badala yakufanya kazi kwa mazoea.

Pia amewasihi  wasimamizi hao kufanya utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji ya vituo husika na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema

Akizungumza mratibu wa uchaguzi  kutoka Ruvuma Salumu katenda amewataka wasimamizi kusimamia viapo kwa mujibu wa kanuni na amewataka wananchi kushiriki kampeni za uchaguzi kwa vyama vyote kwa usawa ili waweze kusikiliza sera za wagombea na kuwapa nafasi ya kuchagua kiongozi aliye bora

Msimamizi wa uchaguzi kutoka Mbozi Dani mteve  amewataka wananchi kujitokeza  kwa wingi kushiriki katikanuchaguzi 

 

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.