DIWANI MALILO ATOA MSAADA KWA WATOTO WASIOJIWEZA SHULE YA MSINGI BONYOKWA

  Na Angelina Mganga,DmNewsOnline

        Dar es Salaam 


DIWANI wa Kata ya Bonyokwa  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhe.Tumike Malilo ametoa msaada  wa sare za shule ,kalamu na daftari kwa watoto wasiojiweza katika shule ya msingi Bonyokwa

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Januari 29,2026 mara baada ya kukabidhi msaada huo  amesema kwamba ameamua kutoa msaada kwa watoto hao kuonyesha upendo na kujitoa kwa ajili ya jamii inayomzunguka katika  Kata hiyo.

"Nimeona ni vema kuwasaidia watoto wasiojiweza kwa kuwapatia msaada wa sare za shule ili nao watambue kuwa tunawapenda na kuwathamini",amesema Mh.Tumike

Aidha,amesema tunaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Afya,elimu na miundombinu ya Barabara.


                  Sekta ya Elimu
 
Akizungumzia sekta ya elimu Diwani huyo amesema kwamba  katika Kata ya Bonyokwa Ina shule Mbili za msingi ambazo ni Shule ya Msingi Kifuru na Bonyokwa ,Hali ya shule ya msingi Bonyokwa  tumeongeza madarasa sita,matundu 15 ya vyoo na changamoto iliyopo kwa sasa shule inahitaji uzio pamoja na madawati.

Watoto waliojiunga na darasa la kwanza shule ya msingi Bonyokwa ni 212 ambapo kifuru ni 250 kwa matokeo ya wanafunzi wa darasa la nne wamefanya vizuri katika mitihani yao.

Kata ya Bonyokwa ipo shule Moja ya Sekondari na High School ambayo ujezi wake unaendelea na ujenzi wake umefikia asilimia 95 na Ina madarasa 53,Ina maabara zote tatu za fizikia,biolojia na kemia na imejitosheleza Kwa Kila kitu.

Akizungumzia sekta ya Afya Mhe.Diwani Tumike amesema ipo Zahanati katika Mtaa wa Kisiwani na Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kujenga jengo la kupumzikia wagojwa,wajawazito na kupimia watoto.


"Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutuwezesha katika kata yetu na kwa mwaka wa fedha 2025/26 tayari zimeshatengwa milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya.

Pia amesema kwamba kata ya Bonyokwa imeendelea kuimarisha ulinzi shirikishi na mpaka sasa ujenzi wa kituo cha Polisi cha kata umefikia asilimia 75 ujenzi unaendelea vizuri uko katika hatua za mwisho kukamilika

Hali ya miundombinu ya Barabara katika Kata ya Bonyokwa kulikuwa hamna barabara zenye kiwango cha lami lakini tunamshukuru Rais Samia na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa Tarura hasa kwa mtaa wa Msingwa kulikuwa na changamoto ya daraja lakini kwa sasa daraja limejengwa kwa kiwango cha zege lakini pia mkandarasi anaendelea  na ujenzi wa Barabara ya Segerea Bonyokwa  kwa mita mia saba anaendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami na taa za barabarani.   


Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.