WAUMINI WA KANISA KATOLIKI WAPINGA KAULI ZILIZOTOLEWA NA ASKOFU RUWA'ICHI
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
WAUMINI wa Kanisa Katoliki,Mackdeo Shilinde na Gerald Abel wanapinga hadharani kauli zilizotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Jude Thaddaeus Ruwa'ichi wakati wa homilia ya Misa Takatifu ya Krismasi tarehe 25 Desemba 2025 wakisema mimbari imegeuzwa jukwaa la matusi,hukumu na vitisho badala ya Injili ya mapendo .
Katika taarifa ya waumini hao wamesema maneno makali yaliyotamkwa madhabauni katika homilia ya Misa ya Krismas ,Askofu Ruwa'ichi alitumia maneno mazito kama "lofa", "mpumbavu", "njaa njaa", "msaliti" na Ndumilakuwili", wakisema kauli hizo zinakiuka mafundisho ya Biblia.
Waumini hao wamesema "Biblia inaonya wazi dhidi ya matumizi ya lugha ya matusi na hukumu huku wakinukuu maandiko Matakatifu"Msihukumu ,msije mkahukumiwa", (Mathayo 7:1)
Katika msimamo wao,waumini hao wamesema mimbari imewekwa kwa ajili ya kuhubiri Neno la Mungu,kuimarisha Imani ya waumini,kuwafariji wenye huzuni na kuwaongoza waumini katika njia ya mapendo,uvumilivu,mshikamano na amani"
Wamenukuu"Heri wapatanishi,maana hao wataitwa Wana wa Mungu",(Mathayo 5:9)
"Jitahidini kuuhifadhi Umoja wa Roho katika kifungo cha amani",(Waefeso 4:3).
Aidha ,waumini hao wamesema kauli za matusi zinawakwaza waumini kinyume na onyo la Biblia linalosema:"Msikwazane wadogo Hawa",(Mathayo 18:6) kauli hizo hazikujibu hoja hata moja zilizowasilishwa kwa mamlaka za juu za Kanisa kujibu barua ya waumini Stanislaus Nyakunga na Elia Phaustine kwa Balozi wa Vatican.
Barua hiyo ilikuwa ni ombi la tathmini ya mwenendo wa Padri Charles Kitima,Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC),anayelalamikiwa na kuhusishwa na siasa.
Kwa mujibu wa waumini hao,badala ya hoja kujibiwa kwa busara au kufanyiwa uchunguzi wa kikanisa walishuhudia waumini wakiburuzwa hadharani kwa maneno ya dharau.
Waumini hao wamesema kwa msimamo mkali kwamba Kanisa Katoliki halipaswi kuingizwa katika siasa za chama chochote wakisisitiza kuwa Padri au Askofu anapaswa kuwa muunganishi wa waumini na Taifa ,si mshauri wa chama Cha siasa.

Comments
Post a Comment