SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUFUATILIA VITAMBULISHO NIDA KWAKUTUMIA SIMU ZA VIGANJANI.

Timothy Marko DmNews Online 

          DAR ES SALAAM. 

SERIKALI imewataka Wananchi kuweza kutumia simu za viganjani kwa kupiga namba 15274 ilikuweza kupata kwa urahisiVitambulisho vya Taifa.

Akizungumza Leo Desemba 29,2025 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amesema kuwa kwa kutumia Namba hiyo kutamuwezesha Mwananchi kupata taarifa za Vitambulisho hivyo na Majibu yake kwa Muda wa siku Tano.

"Kwakutumia namba hii utapata taarifa ya kitambulisho chako kama kimeteng'enezwa,Nakusisitiza Vitambulisho Vilivyoharibika watavipata Febuary 2026" Amesema Simbachawene

Ameongeza kuwa Serikali imepanga mkakati wa matumizi ya kitambulisho kimoja kwaajili ya Matumizi yahuduma za kiserikali.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa Ajira kwa maafisa wapya kupitia Mamlaka hiyo kwa Ngazi ya Wilaya na Kata.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) James Kaji amesema kuwa Awali taasisi hiyo ilianzisha mfumo wa kupata Vitambulisho hivyo kwenye Wilaya. 

Amesema kumekuwa na tatizo mrundikano wa Vitambulisho Vingi ilikuweza kukabiliana tatizo hilo, Anaekuja kuchukua Kitambulisho itamlazimu kuchukuliwa Alama za Vidole ili kuhakiki taarifa zake .

"Endapo Umesahau kitambulisho chako utaulizwa jina la Muombaji sambamba na jina la Mwisho la Mama" Amesema Kaji. 

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.