WAZIRI MKUU DKT.NCHEMBA :AKEMEA WATUMISHI WAZEMBE, WALA RUSHWA ATOA MAELEKEZO.
Na Mwandishi wetu, DmNewsonline
DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewaeleza watanzania kuwa Serikali haitokuwa na mzaha na Watumishi wa Wazembe, Wavivu na Wala rushwa na kwamba ikithibitika Mtumishi anafanya makosa hayo na anakwamisha utendaji asiishie kuhamishwa bali afukuzwe kazi kabisa.
Waziri mkuu Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo leo Novemba 25,2025 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari, pamoja na Waandishi wa habari.ambapo amesema.
“kuhusu nidhamu kazini hatutokuwa na mzaha nalo, uadilifu hatutokuwa na mzaha nao, bila nidhamu na uadilifu hatutotimiza malengo yaliyopo kwenye dira na Ilani, na nimewaelekeza Watendaji wa Serikali wasiwe na mzaha kwenye hili, na wale Wazembe, Wavivu, Wadokozi, Wala rushwa tutashughulika nao”amesema Dkt Nchemba
“Nimeelekeza Mtumishi Mzembe na Mla rushwa asihamishwe kituo Cha kazi akibainika na kuthibitika afukuzwe, hatuna uhaba wa Vijana wa kufanya kazi”
“Mh. Rais ameelekeza utaratibu wa kuwasikiliza Watanzania, na hili tumeshaelekeza kote kitakachofuata tutafuatiliana, ni kweli kuna baadhi ya maeneo kunakuwa na ulegevu wa utimizaji wa majukumu ya namna hii”amesisitiza Waziri Mkuu 













Comments
Post a Comment