WATANZANIA MSIKUBALI KUYUMBISHWA KUINGIZWA KATIKA MACHAFUKO’
Mwandishi wetu,DmNewsonline
WATANZANIA wameshauriwa wasikubali kuyumbishwa na wanaharakati ambao wenyewe wapo kwa ajili ya kuiona nchi ya Tanzania inavurugika na kukosa utulivu.
Ushauri huo umetolewa leo Novemba 30 ,2025 jijini Dar es salaam na wanaharakati huru ambao wamemua kueleza hatua kwa hatua mbinu chafu ambazo zinatumiwa na baadhi ya wanaharakati ambao wamekuwa wakitafuta mbinu mbalimbali kuvuruga amani ya Tanzania.
Wamesema kuwa sababu kubwa ya vurugu ambazo zinatengenezwa na wanaharakati hao wenye nia ovu na Taifa la Tanzania ni kutaka kuvuruga kasi ya ukuaji wa maendeleeo ambayo imekuwa tishio kwa baadhi ya nchi jirani.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mwanaharakati Huru Ahmed Kombo amebainisha kuwa tangu kuazishwa kwa vyama vingi nchini mwaka 1995 baadhi ya wanaharakati na vyama vya siasa vya upinzani vimekuwa vikilalamikia tawala zote ambazo zinapita katika uongozi wa nchi yetu.
Amesema kuazia utawala wa Awamu ya Tatu chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Hayati Benjamini Mkapa, Dkt.Jakaya Kikwete, Hayati Dkt.John Magufuli ,na kwa upande wa Zanzibar na hata leo wamekuwa watu wa kulalamika tu.
Kombo amesema katika vurugu zilizojitokeza hivi karibuni zimechagizwa na makundi ya watu ambao walipokea malipo kutoka taasisi za nje ambazo zinafanya shughuli kwenye nchi zinazozunguka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na moja ya taasisi hizo ni Ford foundations.
“Taasisi hiyo iliwahi kulalamikiwa huko nyuma na Rais wa nchi Jamhuri ya watu wa Kenya na kwa Tanzania taasisi hiyo imeshatoa zaidi ya sh bilioni tano kwa taasisi sita ili kuratibu vurugu zilizojitokeza hivi karibuni.
"Ndugu zangu hapa ndio nataka niseme kuwa haya yote ambayo wanayafanya lengo lao nikutaka kuvuruga amani ,utulivu , mshikamo uliyopo katika nchi yetu."amesema Kombo
Kwaupande wake Yona Joseph Wachalinze amesema serikali iwe macho na kauli za viongozi baadhi wa vyama vya Siasa Nchini.
“Mfano haya yaliyotokea ni ya kiongozi mkuu wa Chama cha Siasa hapa kinachopewa ruzuku ya mabilioni ya fedha zinazotokana na kodi ya watanzania ambaye alisema kuwa katika Uchaguzi mkuu mwaka huu watakinukisha na jambo ambalo limetokea
Ameongeza kuwa hayo yote yanayoonekana ni wivu wa Maendeleo kutokana na miradi mikubwa iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa nchini Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
“Hivyo yote haya yanafanywa na wanaharakati na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanadhamaniwa na taasisi za nje na ndio maana vijana wa vyama vya Siasa ambao tunajua maisha yao yalikuwa magumu na wengine ni watoto yatima leo wanalazwa kwenye hotel za five star Nairobi .”
Amesisitiza watu hao wanalipwa na kulala bure kwenye hizo hotel na kazi yao ni moja tu kuchafua taswira ya nchi yetu, lengo lao ni kuichafua nchi na kuhakikisha miradi mikubwa haiendi .
Kuhusu mjadala uliojitokeza kupitia Bunge la Umoja wa Ulaya lenye nchi 27 kati ya nchi 44 za Ulaya ,Yona amesema hata kama umoja huo hautasaini dokezo la bilioni 400 halitaathiri bajeti ya Tanzania ya Sh.Trilioni 56 ambapo kwakifupi unaweza kuona bunge hilo la umoja wa Ulaya linachangia kama asilimia 0.7.
Amefafanua kitakachoathirika kwa nchi yetu ni wale development partners (wadau wa Maendeleo kwa upande wa mijini na vijijini ambapo watanzania wengi wanazijua kama NGO,s.
Hata hivyo Serikali bado wanaendelea na mazungumzo ya kidplomansia kuhusu mjadala huo ulioibuliwa kupitia bunge hilo.













Comments
Post a Comment