MSAMA: TUWAPUUZE WANAOLIPWA KUVURUGA AMANI YETU

 Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline

                    DAR ES SALAAM 

MKURUGENZI wa Msama Promotions na Mfanyabiashara malufu nchi Tanzania  Alex Msama amewataka Watanzania kuwapuuza watu ambao wanalipwa ili kuvuruga amani ya nchi yetu ya Tanzania.

Amesema maranyingi watu wanaofanya hivyo sio Watanzania na baadhi yao ni Watanzania wanaoishi nje ya nchi kama vile nchi jirani na Tanzania pamoja na mataifa mengine ya nje.

"Watanzania wenzangu, nawasihi kwa moyo mmoja tuwapuuze watu wanaotaka kuvuruga amani yetu, maana watu hawa wanalipwa Mamilioni ili kuvuruga amani yetu tuliyo nayo."amesema 

" Miongoni mwa watu hawa hawaishi hata hapa nchini bali wanaishi nje ya nchi na wengi sio Watanzania na wanalipwa na baadhi ya Watanzania na watu wengine wa nje ya nchi ili wavuruge amani yetu iliyoasisiwa na wazee wetu."amesisitiza 

Nakuongeza kuwa, watu wanaofanya hivi furaha yao nikuona amani yetu inavurugika ili watuibie rasilimali zetu, pia furaha yao ni kuona tunagombana, tunauana na kuchukiana, tuwapuuze"   



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.